Waziri
wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Warajis Wasaidizi wa mikoa
ya Tanzania Bara leo 6.1.2021 katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi
yakiwemo magari pamoja na kompyuta katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya
Ushirika Jijini Dodoma.
Mrajis
Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson
Ndiege akitoa taarifa wakati hafla ya kukabidhi vitendea kazi yakiwemo
magari pamoja na kompyuta katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Jijini Dodoma.
Sehemu ya Warajis kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda leo Jiji Dodoma.
Waziri
wa Kilimo Prof.Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi kompyuta mpakato
(laptop)Afisa Ushirika wa Mkoa wa Geita Dorah Mwabeza(Kushoto)kwa niaba
ya Mrajis wa Mkoa huo.Prof. Mkenda amekabidhi laptop 20 pamoja na
kompyuta za kawaida 50 zilizotolewa naTume ya Maendeleo ya Ushirika leo
6.1.2021 jijini Dodoma kwa warajis.Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege
Waziri
wa Kilimo Prof.Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi funguo za gari
Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Simiyu Ibrahimu Kadudu
(Kushoto).Prof. Mkenda amekabidhi magari matano yenye thamani ya milioni
275/= yaliyotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika leo 6.1.2021 jijini
Dodoma Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Dkt.Benson Ndiege
Waziri
wa Kilimo Prof. Adolph Mkenda (Katikati) akimkabidhi funguo ya gari
Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Kilimanjaro Henjewele John
(Kushoto.
Waziri
wa Kilimo Prof. Adolph Mkenda (Katikati) akikimkabidhi kompyuta mpakato
(laptop)Mrajis Msaidizi wa Vyama Vya Ushirika Mkoa wa Njombe
Bi.Consolata Kiluma (Kushoto).Prof. Mkenda amekabidhi laptop 20 pamoja
na kompyuta za kawaida 50 zilizotolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika
leo 6.1.2021 jijini Dodoma.Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo
ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege
Sehemu
ya magari manne aina ya Nissan Hard N 300 Double Cabin 4WD yenye
thamani ya Shilingi 275,091,670/- kwa pamoja yalikabidhiwa kwa Warajis
Wasaidizi wa mkoa wa Simiyu, Kilimanjaro, Njombe na Dar es Salaaam na
gari moja lililotumika kwa mkoa wa Kigoma.
Na Alex Sonna, Dodoma
SERIKALI
imeahidi kuendelea kutatua changamoto ya vitendea kazi kwa watumishi
Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini(TCDC) ili wafanye kazi kwa ufanisi
na kurejesha hadhi na heshima ya ushirika nchini.
Sambamba na hilo, imeapa kutofumbia macho mtu yeyote atakayebainika kuchezea fedha za ushirika.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda hafla ya
kukabidhi magari matano na komputa 70 kwa ajili ya kurahisisha utendaji
kazi kwa watumishi wa Tume hiyo.
Amesema
anafahamu watumishi hao wanafanya kazi kwenye mazingira magumu hivyo
serikali inapambana ili kuhakikisha wanaondoa kero zinazowakabili.
Hata
hivyo ameeleza bado kunahitajika mapambano ya wizi na ubadhirifu kwenye
vyama vya ushirika licha ya kuonekana kupungua kutokana na jitihada
zilizofanywa na serikali za kurudisha mali za ushirika.
“Hatutachekeana
na mtu anayecheza na mali za ushirika kwasababu ukifanya hivyo
unakatisha watu tamaa, watakuwa hawana hamu ya kujiunga na ushirika,
Warajis Wasaidizi tusimame kidete kwenye hilo,”amesema.
Pia
amesema licha ya ubadhirifu kupungua lakini bado kuna tatizo la vyama
kushindwa kuandaa vyema hesabu zake na kusababisha kukosa hati safi.
Kuhusu
Sheria, Waziri huyo amesema kuna kazi ya kurudisha imani za watu kwenye
ushirika kwa kupitia upya Sheria ya Ushirika na tayari kazi
imeshaanza.
Awali
Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo ambaye pia ni Mrajis wa Vyama vya Ushirika
nchini, Dk.Benson Ndiege, amesema Tume itaendelea kupambana na kero
zinazoukabili ushirika ikiwamo ubadhirifu na uongozi mbovu kwenye vyama
hivyo.
Aidha,
Dk.Ndiege amesema Tume ipo kwenye mpango wa kuimarisha ofisi za
ushirika nchini na itahakikisha kila mkoa una gari kabla ya mwaka wa
fedha 2020/21 kukamilika.
“Leo
kwa kutumia mapato ya ndani Sh.Milioni 275 zimenunua magari manne
ambayo yataenda kwa Warajis wa mikoa ya Dar es salaam, Simiyu,
Kilimanjaro na Njombe na pia tutatoa gari moja kwenda Kigoma kutokana na
umuhimu wa kilimo cha michikichi,”amesema.
Aidha amesema wamegawa komputa 70 ambapo kati ya hizo 20 ni komputa
mpakato(laptops) ambapo komputa 50 zimetolewa na Benki ya CRDB na hizo
zingine zimenunuliwa kwa mapato ya ndani.