Prof.ndalichako asema tanzania imejizatiti kuondoa fikra potofu kuhusu masuala ya kijinsia

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akizungumza katika ufunguzi wa semina
ya kimataifa ya kuwajengea uwezo vijana wa kike (Girl Guide)juu ya
uongozi ijulikanayo kama Juliette Low Seminar iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.

Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako na Prof Martha Qorro ambae ni
Mwenyekiti wa Chama cha Girl Guides Taifa wakifurahia ngoma kutoka kwa
wanafunzi wa shule ya msingi Diomond (hawapo pichani)wakati wa ufunguzi
wa semina ya kimataifa ya kuwajengea uwezo vijana wa kike juu ya masuala
ya uongozi inayofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akipita katikati ya Girl Guides kutoka
Shule ya Msingi Oasis ya Jijini Dar es Salaam mars baada ya kuwasili
kufungua semina ya kimataifa ya Uongozi ya Jls.
Baadhi ya Makamishna na Volunteers
wa Girl Guides Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo
pichani)wakiwa wameshika bendera za nchi mbalimbali wakati wa ufunguzi
wa semina ya kimataifa ya kuwajengea uwezo vijana wa kike juu ya uongozi
iitwayo Juliette Low Seminar Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akinunua kikoi katika duka la Juliette
Low Seminar kuashiria ufunguzi wa duka hilo wakati wa ufunguzi wa semina
ya kimataifa ya kuwajengea uwezo vujana wa kike juu ya masula ya
uongozi jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiwa kwenye picha ya pamoja na Girl
Guides wa shule ya msingi Oasisi ya jijini Dar es salaam mara baada ya
kufungua semina ya kuwajengea uwezo vijana wa kike kwenye masuala ya
uongozi inayofanyika jijini Dar es Salaam.
Girl Guides kutoka shule ya Msingi
Oasis ya jijini Dar es Salaam wakiimba ngonjera mbele ya Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako wakati wa ufunguzi wa
semina ya kimataifa ya kuwajengea uwezo vijana hao iliyofanyika Jijini
Dar es Salaam
Baadhi ya Girl Guides kutoka nchi
mbalimbali wanaoshiriki semina ya kimataifa ya kuwajengea uwezo watoto
wa kike juu ya masuala ya uongozi ijulikanayo kama Juliette Low
inayofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako wakati wa ufunguzi
wa seminia hiyo .
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na
washiriki wa Semina ya kimataifa ya uongozi ijulikanayo kama JLS
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
………………….
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema Tanzania ni miongoni mwa
nchi ambayo imejizatiti na ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha kwamba
inaondoa fikra potofu kuhusiana na masuala ya kijinsia.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo
jijni Dar e Salaam alipomuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan katika ufunguzi wa Semina ya Kimataifa ya kuwajengea uwezo vijana
wa kike (Girl Guides) katika masuala ya Uongozi ijulikanayo kama
Julitte Low Seminar.
Amesema lengo la semina ni kupanua
na kuimarisha ushiriki wa wasichana katika masuala ya girl guides
lakini pia kuwawezesha kushirikiana katika masula ya kiutamaduni na
uongozi ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo wasichana hao ili wazidi kufanya
vizuri zaidi katika Jamii wanazotoka.
“Naamini baada ya semina hii ya
siku saba wasichana watakuwa na uwezo kushiriki katika masuala ya
uongozi na kukemea imani potofu ambazo zinakuwa zikionesha kuwa mwanamke
ni kiumbe dhaifu na kutengeneza mtazamo chanya kuwa wanawake ni viumbe
kama wanaume na wana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko katika ulimwengu
huu,”Alisema Prof Ndalichako.
Prof Ndalichako amesema Nchi ya
Tanzania inatekeleza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia na kuwa
katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawake na wanaume wana fursa
sawa katika maendeleo.
“Mhe Makamu wa Rais Mama Samia
Suluhu asingeweza kupata nafasi aliyo nayo kama nchi ingekuwa bado ina
dhana potofu , uwepo wake ktk nafasi ya Makamu wa Rais, viongozi na
wataamu wengine katika nyanja mbalimbali inaonesha kuwa nchi yetu
imepiga hatua katika kuweka usawa wa kijinsia ”aliongeza Prof ndalichako
Amewapongeza Waandaaji wa Semina
hiyo kwa kuchagua Tanzania kuwa nchi mwenyeji na kwamba Tanzania ina
historia ya kutoa wanawake ambao ni wa nguvu akiwataja viongozi hao kwa
uchache kuwa ni marehemu bibi Titi Mohamed ambaye amekuwa kiongozi wa
nchi yetu wakati wa uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Getrude Mongela ambaye alishiriki kwenye mkutano wa
Beijing, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro, Spika Mstaafu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna makinda na sasa Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Girl
Guides Taifa Prof Martha Qorro amesema semina ya mafunzo ya uongozi kwa
vijana wa kike (Girl Guides) inafanyika ulimwengu mzima na itasaidia
wasichana hao kujitegemea, kujitambua, kujithamini, kupenda taifa lao
kumpenda Mungu kuhesimu wengine na kusaidia mahali popote panapohitaji
msaada.
Kwa upande wake mwakilishi wa Bodi
ya Dunia katika “World Association of Girl Guide and Girl Scout” kwa
kanda ya Afrika Florentina Mganga amesema semina hii inaendelea
ulimwenguni kote na vijana wa kike 700 watapata mafunzo juu wa uongozi
na itawawezesha kujua kuwa mtoto wa kike anaweza kuwa kiongozi
wanachotakiwa ni kujiamini.
Semina ya Kimataifa ya kuwajengea
uwezo vijana wa kike juu ya masula ya uongozi inashirikisha nchi 17
ambazo ni Marekani, Uingereza, Ujerumani Swizaland, Ghana, Zimbawe,
Malawi, Rwanda, Burundi, Kenya, Madagascar, Egypt, Germany,Uganda,
Sierra Leone, Poland, Hong Kong, Philippines na Tanzania ikiwa kama
Mwenyeji wao.