Rais magufuli amtaka makonda arudishe fedha za tasaf alizosema alitumia kwenda dodoma wakati sio masikini

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda kuzirudisha fedha
za TASAF ambazo alizitumia vibaya kwa safari ya kwenda Dodoma ili hali
sio Masikini.


Rais
Magufuli ameyasema hayo hii leo tarehe 17, Febuari, 2020 wakati
akizindua kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mpango wa Maendelo wa
kunusuru Kaya masikini wa TASAF. Hafla imefanyika katika Ukumbi wa Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dsm.

”Kwenye
mpango huu wa TASAF zilijitokeza baadhi ya changamoto, kupitia zoezi la
uhakiki wa Kaya Masikini, lililofanyika kuanzia mwezi Novemba 2015 hadi
mwezi Juni 2017. Tuliweza kubaini uwepo wa Kaya hewa 73,561.”

”Ambapo
Kaya 2234 zilithibitika kuwa wanakaya wake sio Masikini na hapa
nafikiri wakina Makonda ambao walizitumia hizi fedha kwenda safari ya
Dodoma wakati sio Masikini naomba kama hili ni kweli Makonda azirudishe
hizi fedha. Kama ni kweli alitumia fedha za TASAF akaenda nazo huko
alipokuwa anaeleza, na yeye hausiki kwenye Kaya Masikini mkae
muziangalie hizo fedha lazima azirudishe.”

Kabla
ya Rais kutoa kauli hiyo, Makonda alisema mwaka 2012 alipewa nauli na
Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kwenda mkoani Dodoma kugombea makamu
mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM). Amesema
fedha hizo zilikuwa sehemu ya mfuko


“Namshukuru
sana mzee Mkapa kuona bado anaendelea kufanya kazi yake, naomba Rais
Magufuli niseme mbele yako mfuko huu wa Tasaf nami nimenufaika nao,
haikuwa moja kwa moja.”

“Lakini wakati naomba nafasi ya  makamu mwenyekiti wa vijana (UVCCM)
Mkapa ndio aliyenipa nauli ya kwenda kuomba kura Dodoma. Kwa hiyo
naimani ilikuwa sehemu ya huu mfuko, alikuwa na moyo,” alisema Makonda.