Rais magufuli awavaa tena viongozi wa mkoa wa dar es salaam ” yanafanyika mambo ya hovyo, huwezi kuamini kama kuna viongozi kwenye huu mkoa”

Rais
Magufuli amesema mambo ya hovyo  yanayofanyika katika mkoa wa Dar es
Salaam yanamfanya ajiulize kama mkoa huo kuna viongozi.


Magufuli
aliyasema hayo jana Jumapili Septemba 22, 2019 wakati akiwaapisha Ikulu
jijini Dar es Salaam viongozi mbalimbali aliowateua Ijumaa iliyopita ya
Septemba 20,2019.

Miongoni
mwa miradi ambayo Rais Magufuli ameonyesha kutoridhishwa nayo ni ya
uboreshaji wa ufukwe wa Coco uliopo Manispaa ya Kinondoni.

Meya wa Manispaa hiyo ni Benjamin Sitta na mkuu wa wilaya hiyo ni Daniel Chongolo huku mkoa huo ukiongozwa na Paul Makonda.

Magufuli
amehoji kitendo cha Meya wa Manispaa hiyo kumkabidhi mkandarasi mradi
huo wa Coco ambao unaingiliana na ujenzi wa barabara inayopita baharini
ya Salender.

Rais
Magufuli aliwachambua viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wakati akijenga
hoja kuhusu viongozi wa mkoa wa Morogoro walioshindwa kusimamia
majukumu yao ipasavyo na kuwataka viongozi wenye dhamana kuwatumikia
wananchi wanaowaongoza.
Alisema
Dar es Salaam yanafanyika mambo ya hovyo, huwezi kuamini  kama kuna
viongozi, “Baada ya kutembelea machinjio ya Vingunguti, siku moja baadae
nimeona kwenye TV Meya anakwenda kumkabidhi Mkandarasi site, ni mambo
ya ajabu, Meya na kukabidhi site kwa Mkandarasi ni wapi na wapi?
Mkandarasi mwenyewe ni yule aliyejenga soko la Mwanjelwa na akashindwa”

Rais
Magufuli ameeleza kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, huwezi ukajenga
muundo mkubwa ndani ya mita 60 kutoka baharini au ziwani, lakini
chakushangazwa alipokabidhiwa kuna mradi mwingine wa ujenzi wa daraja la
Salender.

“Mradi
huu wa Salender una barabara nne kuna nyingine inatoka Hospitali ya Aga
Khan inapita katika daraja inakwenda hadi Coco Beach. Kibao kipo sasa
unajiuliza miradi yote ni ya Serikali, huu mradi ,mkubwa tulitoa
Sh200bilioni utapita wapi?

“Je
watajenga muundo wa hoteli pale, je wale wachuuzi watafukuzwa. Mradi
wowote ambao ni positive kwa watu lazima uwatafutie njia mbadala, lazima
uwapeleke mahali ili mradi ukikamilika warudi,” amehoji.

Amesema
Coco Beach haiwezi kujengwa kwa Sh14 bilioni, wakati kinachotakiwa ni
kutengeneza njia sanjari na  kuweka vitu vya kukalia  kuwapa fursa ya
watu wanaotaka ufukweni, kumpumzika.