Rais magufuli : kazi za uongozi zinahitaji uvumilivu…utasemwa,utachafuliwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewataka viongozi aliowaapisha
leo Jumapili Oktoba 20,2019 Ikulu kuwa wavumilivu na wasihofie
kuchafuliwa na watu, bali wajikite zaidi kwenye kutekeleza wajibu wao
kama watumishi wa Umma.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es salaam wakati
akiwaapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na
Balozi, ambapo kazi ya uongozi inahitaji uvumilivu.

“Kazi za uongozi zinahitaji uvumilivu, zinahitaji kumtanguliza Mungu
mbele, utasemwa, utachafuliwa lakini ndiyo kazi ya uongozi, naombeni
katimizeni wajibu wenu kaangalieni haki, kaangalieni sheria kwa ajili ya
kuwatumikia wananchi wote”,
amesema Rais Magufuli
“Kazi hizi ni lazima tuwatumikie wananchi wanyonge, juzi nilikuwa
Mtwara kaimu wa TAKUKURU anafahamu tulikuta malalamiko kuhusu kulipwa
korosho,baada ya kumuagiza amekuta vyama ushirika 32 vilivyokuwa
vinawadhulumu , wananchi wameibiwa Bil. 1. 2”,
amesema Rais Magufuli.