Rais magufuli kuanza ziara ya kikazi visiwani zanzibar leo

Rais
Magufuli aliyekuwa mapumzikoni nyumbani kwake, Chato mkoani Geita
amewasili jana Alhamisi Januari 9, 2020 jijini Dar es Salaam.


Mara
baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam akiwa na mkewe, Janeth, Rais Magufuli alisalimiana
na baadhi ya wafanyakazi katika uwanja huo.

Taarifa
iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu ya Tanzania,
Gerson Msigwa amesema leo  Ijumaa Januari 10, 2020 Rais Magufuli ataanza
ziara ya kikazi ya siku tano visiwani Zanzibar.