Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Mary Masanja (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Rawan Dakik (wa
nne kutoka kushoto) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika
kutangaza Mlima Kilimanjaro, katika hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro . Mhe. Mary Masanja pia amemtangaza
Rawan kama Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro. Wanaoshuhudia ni Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella(wa nne kutoka kulia) wazazi wa
Rawan, Mbunge wa Arusha Mjini,
Mhe. Mrisho Gambo(wa tatu kutoka kulia),Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,
Mhe.Jerry Muro (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TTB ,
Betrita Lyimo (kulia)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Mary Masanja (kushoto) akimkabidhi ua Rawan Dakik (katikati) ikiwa
ni ishara ya kumkaribisha baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro akitokea bara la Asia alikopanda Mlima Everest.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Mary Masanja (kulia) akiteta jambo na wazazi wa Rawan kabla ya
hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro. Mhe. Mary Masanja pia amemtangaza Rawan Dakik kama Balozi
wa hiari wa Mlima Kilimanjaro.
Wizara ya Maliasili na Utalii imemteua
Rawan Dakik kuwa balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kutambua
jitihada zake za kutangaza Mlima Kilimanjaro, baada ya kupanda mlima
huo kwa takriban mara tano na pia kuipeperusha bendera ya Tanzania
katika kilele cha mlima mrefu zaidi duniani Everest uliopo bara la Asia.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema
hayo leo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Rawan Dakik yaliyofanyika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro leo.