Rc gambo awaonya wenyeviti wa mitaa vijiji na vitongoji

Moja ya wananchi akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo(hayupo pichani) akieleza na kuomba Serikali kuangalia hatma yao kwani wao
wanategemea eneo hilo kuendesha maisha yao kama walivyokutwa na kamera
ya matukio jijini Arusha.
Sehemu ya makazi ya wananchi wa eneo la Loswira kata ya Moshono ambao
Jana mkuu wa mkoa wa Arusha alipita kukagua mipaka yao na JWTZ kikosi
Cha 977 kj kwenye mgogoro uliodumu kwa muda mrefu picha na Ahmed Mahmoud
Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipata maelezo kutoka kwa viongozi
wa JWTZ wakati walipofika kukagua mipaka ya eneo hilo ikiwa ni kujionea
na mwisho kutoa maamuzi ya mgogoro huo.

Wananchi wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakiwa na
viongozi wa JWTZ wakikagua maeneo ya wananchi waliovamia eneo la jeshi
ambao Jeshi hutumia kwa mazoezi.
Add caption
Moja ya nyumba za wakazi eneo la Losirwa kata ya Moshono kama
zilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha picha zote na Ahmed
Mahmoud Arusha.
Moja ya wananchi akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo akieleza na kuomba Serikali kuangalia hatma yao kwani wao
wanategemea eneo hilo kuendesha maisha yao kama walivyokutwa na kamera
ya matukio jijini Arusha.
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkuu wa
mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesitisha kwa muda kuendelea na shughuli
yeyote kwenye eneo la Losirwa kata ya Moshono hadi Serikali itakapotoa
maelekezo Mengine ambapo amewaonya Wenyeviti wa Mitaa kuacha kuchukuwa
fedha na kutoa vibali vya Ununuzi wa Ardhi kwenye maeneo yenye Migogoro.

Aidha
Amezitaka halmashauri za wilaya kuacha kutoa vibali vya ujenzi kwa
wananchi kwenye maeneo yenye migogoro kwa kuwa inaleta mikanganyiko
kwenye jamii na kuleta ugumu wakati wa kuitatua.

Gambo
ametoa kauli hiyo Jana wakati alipotembelea kuona eneo lenye mgogoro
baina ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi Cha 977 kj na
wakazi wa eneo la Losirwa kata ya Moshono jijini Arusha uliodumu kwa
muda mrefu Sasa.
Akiongea
Mara baada ya kukagua eneo hilo na kusikiliza pande zote ametoa maagizo
hayo na kueleza kuwa wananchi waendelee kuwa watulivu hadi Serikali
itakapotoa maelekezo mapya kufuatia mgogoro huo.
Alisema
kuwa wananchi wengi wanajielewa kama Kuna mtu anaendelea na ujenzi
aaxhie hapo hapo hadi Serikali itakapotoa maelekezo mapya.
“Tunaunda
tume ya wataalamu kupitia upya na watatoa mapendekezo baada ya taarifa
ndipo tutatoa maamuzi lakini kwa Sasa shughuli zote nimezisitisha”
Alibainisha
kuwa Wenyeviti na Tarafa na vijiji wanaopitishia watu vibali vya
kununua Ardhi watawachukulia hatua za kisheria kwani wao ndio chanzo Cha
kuwaingiza wananchi kwenye migogoro.
Kwa
Upande wao wananchi wa eneo hilo Regina Elias na Poulo Mollel
wakizungumza wameitaka Serikali kuangalia suala hilo kwa kina na kufanya
Tathmini upya kwani wao wameishi muda mrefu eneo hilo na wanategemea
maeneo hayo kwa kujipatia riziki zao za kila siku.
Walisema
kuwa fedha walizopata kama fidia bado hazilingani na maeneo yao utakuta
mtu amelipwa kiasi kidogo na mwingine amelipwa eneo kama hilo kiasi
kikubwa kwa eneo lenye ukubwa kama huo na Tathmini imekaa muda wa miaka
sita ndipo malipo yamekuja kulipwa bila maandishi yeyote hali inayoleta
mkanganyiko kisheria.
“Tunaiomba
Serikali yetu kwa kuwa sisi tunategemea kilimo na tumeishi muda mrefu
1960 jeshi limenikuta hapa huku jina langu likiwa halipo kwenye orodha
ya malipo naambiwa nikae kifamilia kwani kwenye familia Kuna malipo ya
fidia kwenye eneo langu naomba mkuu wa mkoa tuangalie kwenye suala
hilo”alisema Martha John bibi mwenye miaka 86.