Rc shigella awaagiza ma dc kufanya uzinduzi wa vifurushi vya bima ya afya kwenye wilaya zao

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa NHIF Anna Makinda akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MKURUGENZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga akizungumza wakati wa uzinduzi huo

MWENYEKITI wa Chama cha Bodaboda Tanzania Michael Haule akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa NHIF Anna Makinda kushoto akipokea cheti kutoka kwa
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kwa kutambua mchango wake
kutokana na uhamasishaji ambao wanaufanya wakati wa uzinduzi huo
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga kushoto akipokea
cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
kwa kutambua mchango wake kutokana na uhamasishaji ambao wanaufanya
Msanii Mrisho Mpoto maarufu Mjomba akichangia fedha wakati wa uzinduzi huo
WATUMISHI
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakicheza wakati wa uzinduzi
huo kushoto ni Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga Ally Mwakababu katika ni
Isaya Shekifu ambaye ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha na kulia ni
Meneja wa NHIF Mkoa wa Kilimanjaro

 Sehemu ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga

MKUU
wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella amezindua rasmi kampeni ya
uhamasishaji wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya kwenye
viwanja vya Tangamano Jijini Tanga huku akitoa maelekezo kwa Wakuu wa
wilaya za mkoa huo na Meneja wa NHIF Mkoa huo Ally Mwakababu kuhakikisha
wanafanya uzinduzi kwenye ngazi ya wilaya.

Shigella aliyasema
hayo kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga wakati wa uzinduzi huo
ambapo aliipongeza NHIF kwa uamuzi wa kuja na vifurushi ikiwemo kufanya
uzinduzi kwa kila mkoa ambao ni ubunifu mkubwa sana wanaoufanya na
utawasaidia watanzania wengi kujiunga na mfuko huo.

Mkuu huyo wa
mkoa aliipongeza pia bodi ya NHIF kwa kuwa na ushirikiana mkubwa wa
kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa unaowezesha mfuko huo kupiga
hatua kubwa za kimaendeleo ikiwemo kutoa huduma nzuri kwa watanzania.

“Mimi
nakufahamu vizuri sana Mwenyekiti wa Bodi kwa kazi nzuri ambazo
unafanya kila mahala unapokabidhiwa hakujawahi kulegalega wala kurudi
nyuma kunasonga mbele tena kwa kasi kubwa na mafanio hongera mama kwa
kazi nzuri lakini pia niipongeze bodi ya NHIF”Alisema

Mkuu huyo
wa mkoa aliipongeza bodi ya mfuko huo kwa kazi nzuri ambao wamekuwa
wakiifanya hata wanapokwenda mikoani kufuatilia maendeleo ya mfuko huo
wamekuwa na ushirikiano mkubwa ambao umekuwa na tija kubwa kwa
maendeleo.

“Lakini nipongeza Menejimenti chini ya Mkurugenzi wao
Benard Konga wamekuwa wakifanya kazi kubwa katika kutimiza majukumu yao
kwa kujituma ndio maana taarifa niliyoipata ni kwamba katika mifuko
inayoenda vizuri na wanachama wanapata huduma kwa wakati na gharama
zinazotokana na wanachjama kupata huduma za afya zinalipwa kwa wakati ni
pamoja na NHIF”Alisema

Hata hivyo aliwaagiza wamiliki wa
viwanda kuhakikisha wanawaingiza kwenye mpango wa huduma ya bima za afya
vibarua wanaofanya shughuli za uzalishaji katika viwanda ili waweze
kuwa na uhakika wa matibabu wao na familia zao.

Alisema kwamba
miongoni mwa kundi lililo sahaulika ni vibarua toka viwandani ambao kwa
sasa wanafikiria waingizwe kwenye mpango huo ili wakati wanapougua
waweze kuwa na uhakika wa matibabu

Mkuu huyo wa mkoa alisema
kundi hilo linafanyakazi kubwa ya uzalishaji lakini lipo kwenye
mazingira magumu ya kazi zao huku hawajui hatma ya afya zao pamoja na
familia zinazowategemea kutokana na kutokuwepo kwenye mfumo huo ambao
unawawezesha kupata matibabu kwa njia ya Bima ya Afya.

“Jambo
lililoanzishwa na NHIF la vifurushi vya bima ya afya ni jema sasa
…nawaagiza MaDC na wamiliki wa viwanda wekeni utaratibu mzuri kwa
vibarua wote wanapatiwa huduma hii ili kuwanusuru na afya zao”Alisema
Shigella.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa
Bodi ya Taifa NHIF Anna Makinda alisema ni mfumo bora ulioanzishwa na
mfuko huo ambao unaweza kuyasaidia makundi mengi ambayo yalikosa fursa
ya kupata huduma hiyo ya afya.

Makinda alisema awali mfuko huo
uliwajali watumishi wa umma pekee huku asilimia kubwa ya watanzania
ambao si watumishi hawakuwa na nafasi ya kujiunga na mfuko huo jambo
ambalo ni hatari kwa ustawi wa afya zao.

“Yapo makundi kama
bodaboda,machinga,na sacos mbalimbali ambazo hazikunufaika na huduma hii
lakini kupitia mfumo huu wa vifurushi naamini kila mmoja anaweza
kujiunga na kunufaika ili kwajengea uhakika wa matibabu yao”Alisema.

Mbali
na hayo pia alisema tayari walishakubaliana na benki ya NMB ili kutoa
mwanya kwa wananchi walio na kipato cha chini waweze kulipa kidogokidogo
ili waweze kujiunga na huduma hiyo.

Naye kwa upande wake
Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga alisema
kwamba watanzania asilimia 34 ndio wapo kwenye mfumo wa bima ya afya
bado safari ni ndefu kuhakikisha kila mtanzania anaingia kwenye bima ya
Afya.

Alisema pia mfuko mwaka hadi mwaka mapato yamezidi
kuongezeka na kuanzia mwaka 2014/2015 hadi kufikia sasa yameongezeka
asilimia 33 hivi sasa wanakusanya Bilioni 502 kutoka kwa wanachama wao.

Alisema
mchango wao kwenye sekta ya afya umeongezeka ambapo kwa mwaka wanalipa
mpaka bilioni 441 ambazo wanatuma kwenye vituo vya kutolea huduma za
afya nchini.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akizundua
kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya
Afya kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga