Red cross yatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko mto wa mbu-arusha

 Kulia
ni Muwakishi wa rais Redcross Taifa Ndg Japhet Shirima akikabidhi
msaada kwa mzee Asanterabi Shoo ambae ni miongoni mwa waathirika wa
mafuriko eneo la mto wa mbu wilayani Monduli kufuatia Mvua zinazo
endelea kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini.
Timu ya chama cha msalaba mwekundu wakiwa katika Kata ya Mto wa Mbu mkoani Arusha.
Dora
Mushi-Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba mwekundu mkoani  Arusha
akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mto wa mbu waliopatwa na madhila ya
mafuriko
.

Na,Vero Ignatus -Arusha
Familia zaidi ya 150 zilizoathiriwa na mafuriko ya mvua katika eneo la mto wa mbu wameiomba Serikali kuwatafutia mahali pa kuishi ili kuweza kujinusuru na adha ya hiyo kufuatia mvua zinazo endelea 
Wakizungumza  baadhi ya wazee na walemavu ambao kwasasa hawana mahala pa kuishi kufuatia adha hiyo  huku wakaiomba serikali kupata eneo salama la kuishi kama wanavyo eleza mzee Asanterabi shoo na bi Mariam Mboya kwamba wao wapo tayari kuhama  kama serikali itawapa eneo la kujenga kwasababu viwanja kwa sasa ni walipo sasa ni bondeni
Akizungumza
kwa niaba ya Rais wa Chama cha  msalaba mwekundu taifa baada ya
kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo magodoro na huduma muhimu
kwa wakina mama vyenye thamani ya shilingi milioni 25,Japhet Shirima anaeleza kuwa wameamua kuwafariji 
watu waliopatwa na mafuriko mto wa mbu kama dhima ya chama chao inasema ni kufanya kazi kwa nguvu ya binadamu

  ”Chama
cha Msalaba mwekundu kimeamua  kuwafariji  watanzania wenzetu ili
kuwapunguzia machungu yaliyowapata kutokana na mafuriko na tumewalete
vitu vichache 
 vya nyumbani kama vile magodoro,ndoo,sufuria ,mablanketi kwaajili ya matumizi ya nyumbani”Alisema

Amewataka
 wananchi kuchukua tahadhari na kuepuka kukaa maeneo hatarishi na wakae
maeneo yaliyo salama zaidi ili kuepuka madhara yanayoweza
kujitokeza,ili  kujikinga na majanga hayo.
 Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha msalaba mwekundu mkoani Arusha Dora Mushi amewasihi wananchi kujiunga  na chama hucho kwani  ni kitengo kisaidizi cha serikali
kinachohamasisha ili kuwafikia watu kwa karibu pale yamapotokea majanga

Amesema
wananchi wanapojiunga katika Chama cha msalaba mwekundu zaidi
wanawashauri namna ya kuishi,kujikinga na majanga kwani ndiyo wanaotoa
huduma ya kwanza kabla pale tatizo linapotokea katika jamii 
“Hivyo
katika Kata hii ya na Mto wa Mbu tumewaweza kuhamasisha wameweza
kujiunga  wanachama 60 na tumetenga siku maalumu kwaajili ya kuja
kuwapatia elimu namna ya kutoa huduma ya kwanza linapotokea tatizo
katika jamii”

Kufuatia
mvua zinazo endelea kunyesha wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari za
makusudi ikiwa ni pamoja na kuhama katika maeneo hatarishi ili
kujiepusha na maafa.