Wadudu mwenye sumu kali wawatesa wanakigoma’nairobi fly’

Na Editha karlo,Kigoma
WADUDU wenye sumu kali maarufu kwa jina la Nairobi Fly wamejitokeza kwa wingi katika Manispaa ya Kigoma na kusababisha madhara ya ngozi kubabuka,kuwashwa na vidonda kwa wakazi wa Kigoma mjini.

Akiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani,Diwani wa kata ya Kigoma mjini kupitia chama cha ACT wazalendo Hussen Kaliyango alisema kuwa wadudu hao ambao ni hatari wamejitokeza kwa wingi sasa hivi katika maeneo mengi ya mjini ambapo wamewadhuru wananchi wengi kwa kuunguza miili yao kutokana na sumu waliyonayo.

“Halmashauri yetu inawasaidiaje wananchi wetu wanaopata madhara sasa hivi kwasababu ya wadudu hao ambao sasa hivi wamekuwa wengi mtaani”alisema

Akijibu swala hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Manispaa ya Kigoma ujiji Mwailwa Pangani amewataka wananchi kuishi mazingira masafi kwa kufyeka nyasi zinazozunguka makazi yao.

“Wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari kwa kuishi sehemu ambazo ni safi wadudu wale wanaishi kwenye nyasi lakini pia huwa na tabia ya kufuata mwanga wa taa”alisema

Baadhi ya wananchi waliopata madhara kutoka na mdudu huyo wamesema kuwa hawana elimu yoyote juu ya kujikinga na mdudu huyo wala tiba yake hawaifahamu.

“Mimi nimeamka jana asubuhi nikajikuta nina muwasho maeneo ya shingoni,nikajua ni kawaida ya mwili tu,leo najiangalia tena nikajikuta nina mishirizi mwekundu inawasha ipo kama nimeungua na moto”alisema

Nikawauliza baadhi ya majirani zangu wakaniambia umetambaliwa na mdudu anaitwa nairobi fly nikabaki nashangaa hata sielewi”alisema Neema Mselemu mkazi wa Mwanga

Naye  Agustino Mwantu mkazi wa mji mwema anasema kuwa sasa hivi wananchi wengi wamebabuka ngozi kwasababu ya mdudu huyo ambaye inasemekana ana sumu kali katika maji maji yake lakini mdudu huyo hang’ati anapokutambaa.

“Tumebabuka ngozi kama unavyotuona sura hazifai zimejaa makovu,mdudu huyu ana sumu kali akikuachia sumu yake unaungua ngozi kama umemwagiwa tindikali,serikali ingetusaidia kutupa elimu dawa za kutumia na pia tujikinge nao vipi watoto mashuleni huko nao wanapata taabu”alisema