Saadan yatumia bilioni 1.1 kusaidia miradi ya kijamii

Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae akizungumza na waandishi wa habari 
Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo akielezea mikakati waliokuwa nayo
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei akizungumza kuhusu namna walivyonufaika na uwepo wa hifadhi hiyo
Afisa
Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae katikati akiwa na
wageni kutoka mataifa mbalimbali waliotembelea hifadhi hiyo
Sehemu ya wageni wakifurahia utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan
Aina ya malazi yanayopatikana kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadan kwa wageni wanaofika kutembelea vivutio mbalimbali
Mamba akiwa pembezoni mto Wami akiota jua kama alivyokutwa ambapo jamii ya Mamba wanapatikana pia kwenye hifadhi hiyo


Wanyama aina ya Viboko wakiwa kwenye maji ndani ya Mto Wami ambao
umepita kwenye hifadhi hiyo ya Taifa ya Saadan kama wanavyoonekana

 Kundi la Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Wanyama aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Aina
ya Makundi ya Ndege ambayo yamejenga kiota kwenye hifadhi ya Taifa ya
Saadan ndani ya Mto Wami ambapo ndege hao huishi pamoja ambao huishi
hapo kwa ajili ya kuijepusha na maadui zao

 Wanyama aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Wanyama aina ya Twiga wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Wanyama aina ya Ngiri wakila majani ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Mnyama Ngiri akiwa anakula majani karibu na bahari ya hindi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Ndege aina ya Fundi Chuma akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Mtalii akifurahia upepo wa bahari ndani ya Taifa ya Saadan

Hifadhi
ya Taifa ya Saadani imetumia kiasi zaidi ya sh Bil 1.1 kwa ajili ya miradi ya
maendeleo kwenye vijiji 11 Kati ya 16 vinavyozunguka hifadhi hiyo kupitia
mpango wa ujirani mwema.

Hayo
yalisemwa na Afisa utalii wa hifadhi hiyo Athuman Mbae wakati akizungumza na
waandishi wa habari walipotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni kujionea shughuli
za utalii.

Alisema
kuwa jumla ya miradi 23 iliyoko kwenye sekta za Afya, Elimu, Maji na Mazingira
imeweza kufadhiliwa na hifadhi hiyo kwa kushirikiana na wananchi.

“Tumekuwa
tukishiriki katika miradi ya ujirani mwema ambapo hifadhi inachangia asilimia 90%
huku wananchi wakichangia asilimia 10% kwa lengo la kuhakikisha wanaweza
kuituza miradi hiyo”alisema Mbae.


Awali
akizungumza Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya
Saadan Prisca Lyimo alisema kwamba alisema maboresho yaliyofanywa kwenye
hifadhi hiyo na serikali ya awamu ya tano yamesaidia kuongeza idadi ya
watalii wan je na ndani.

Alisema maboresho hayo yameongeza
mwitikio wa watanzania kutembelea hifadhi za taifa kutokana na kuboresha
miundombinu ufikaje wake huku watalii wanaweza kufika wakiwemo wa
Zanznzar, Dar na Tanga na maeneo mengine hapa nchini.

“Bado
tunaendelea kuhamasisha watanzania waone umuhimu wa kutembelea vivutio
vya utalii vilivyopo hapa nchini hususani hifadhi ya Kipekee ya Saadani
inayopakana na Bahari ya Hindi”Alisema 

Kwa
upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei alisema kuwa hifadhi
hiyo imeweza kusaidiana na wananchi katika kutatua kero mbalimbali ambazo
zilikuwa zinatukabili.

“Hifadhi
imeweza kutujengea nyumba ya Mwalimu,kusambaza maji kwenye nyumba za ibada
sambamba na ujenzi wa choo chashule ambacho kilikuwa hakitumiki kwa muda mrefu kutokana
na uchakavu”alisema Ngulei.

Nao
baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Saadani wamesema kuwa kuishi kwa jirani na
hifadhi kumekuwa ni neema kubwa kwao kwa kipato sambamba na fursa za biashara.

“Watalii
wengine wakija wanaishi nje ya hifadhi hivyo tunapata kipato kwa kuwauzia
chakula ikiwemo na malazi sambamba na kujifunza tamaduni za kwetu
“alisemaAthuman Said.