Dkt. abbas kuendelea kuwa msemaji wa serikali

Rais 
Magufuli ametaja sababu ya kumteua Dk Hassan Abbasi kuwa katibu mkuu wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akisema ni kutokana na
kufanya kazi nzuri ya kuisemea Serikali bila kuchoka. Kabla ya uteuzi
huo, Dk Abbasi alikuwa msemaji mkuu wa Serikali.


“Dk
Abbas amefanya kazi nzuri kama msemaji wa Serikali, hakuchoka aliisemea
vizuri Serikali, ningependa aendelee tu kuwa msemaji wa Serikali lakini
mahali mtu anapotakiwa kupata promosheni, usimnyime promosheni.

“Ndiyo
maana tumemteua awe katibu mkuu wa wizara hiyo na kwa sasa hivi
ataendelea kuwa msemaji wa Serikali mpaka tutakapopata mwingine na
atakuwa anasema sasa akiwa mkubwa zaidi,” amesema Magufuli.