Waziri wa Nishati,Dkt.Medard
Kalemani,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO wilaya ya Kongwa
Shaban Seif wakati akikagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani
Kongwa wakati wa ziara ya Waziri huyo iliyofanyika leo Julai 27,2021.
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard
Kalemani,akizungumza na wananchi wa Mbande wakati wa ziara ya kukagua
eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika
leo Julai 27,2021.
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard
Kalemani,akimsikiliza Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge,Job
Ndugai wakati akizungumza na wakazi wa Mbande wakati wa ziara ya kukagua
eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika
leo Julai 27,2021.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony
Mtaka,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati,Dkt.Medard
Kalemani, ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa
ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mbande
Bw.Peter Chiumbe akitoa kero ya umeme kwa Waziri wa Nishati,Dkt.Medard
Kalemani,wakati wa ziara ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande
wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.
Meneja wa TANESCO wilaya ya Kongwa
Shaban Seif,akielezea hatua za ujenzi wa Kituo cha Kupooza umeme
kilichopo Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa.
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard
Kalemani,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni
wilayani Kongwa mara baada ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha
kupooza umeme cha Kilovolti 22O kinachotarajiwa kujengwa katika eneo
hilo.
Diwani wa Kata ya Ugogoni
Mhe.Elizabeth Lenjima,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa
Nishati,Dkt.Medard Kalemani,ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha
kupooza umeme cha Kilovolti 22O kilichopo Kijiji cha Machenje Kata ya
Ugogoni wilayani Kongwa iliyofanyika leo Julai 27,2021.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha
Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa wakimsikiliza Waziri wa
Nishati,Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kukagua
eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O
kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Machenje.
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani
,akizungumza na wananchi wa Kibaigwa mara baada ya kumaliza ziara ya
kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O
katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa iliyofanyika
leo Julai 27,2021.
Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika
wa Bunge,Job Ndugai,akizungumza wananchi wa Kibaigwa mara baada ya
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani kumaliza ziara ya kukagua eneo la
ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O katika Kijiji cha
Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa leo Julai 27,2021.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony
Mtaka,akizungumza wananchi wa Kibaigwa mara baada ya Waziri wa
Nishati,Dkt.Medard Kalemani kumaliza ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa
Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O katika Kijiji cha Machenje
Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa leo Julai 27,2021.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius
Emmanuel,akizungumza wananchi wa Kibaigwa mara baada ya Waziri wa
Nishati,Dkt.Medard Kalemani kumaliza ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa
Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O katika Kijiji cha Machenje
Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa leo Julai 27,2021.
Baadhi ya wananchi wa Kibaigwa
wakimsikiliza Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani)
wakati akizungumza nao kuhusu changamoto za umeme mara baada ya
kumaliza ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha
Kilovolti 22O katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani
Kongwa leo Julai 27,2021.
………………………………………………………………………….
Na Alex Sonna,Kongwa
MRADI mkubwa wa
kujenga kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O wenye thamani ya
shilingi bilioni 41.2 unatarajiwa kuanza kujengwa Septemba mwaka huu
Wilayani Kongwa ambao utasaidia upatikanaji wa uhakika wa umeme katika
maeneo hayo.
Hayo yamesemwa leo
Julai 27,2021 na Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani wakati wa ziara
ya kukagua eneo la Ujenzi wa kituo hicho kilichopo kijiji cha Machenje
Kata ya Ugogoni amesema kuwa Mhe.Rais,Samia Suluhu Hassan amesikiliza
kilio cha wakazi wa Kongwa
Amesema kutoka
katika kituo cha kufufua umeme cha Zuzu mpaka Kongwa ni kilometa 122
hivyo ni mbali kiasi ambacho umeme umekuwa mdogo na Dodoma limekuwa
Jiji.
“Kwa heshima yenu
sasa Mheshimiwa Rais amesikia kilio chenu na ameelekeza tujenge kituo
cha kufufua umeme tena umeme mkubwa wa KV 220.Nimekuja kutekeleza agizo
la Serikali hili eneo mlilopendekeza tunawashukuru kwani tunaenda
kutatua tatizo la umeme katika eneo hili nimekuja hapa kutatua hii
kero,”amesema
Amesema katika Mji
wa Kongwa kuna miradi minne inaendelea ambapo ni wa kuleta umeme kwenye
vitongoji,kusambaza umeme katika maeneo ambayo yapo karibu sana mitaa
kama Mbande,kuboresha miundombinu ya umeme pamoja na mradi mkubwa wa
kujenga kituo cha kupooza umeme.
“Yote hayo
yanaifanya Dodoma kuwa na umeme wa uhakikika kuliko maeneo
mengine.Kwenye mradi wa kuboresha miundombinu Serikali imetoa bilioni
2.7 kwenye Jiji zima lakini asilimia takribani 70 inakuja katika Jimbo
la Kongwa,”amesema Dkt.Kalemani
Amesema kituo hicho
kitahudumia maeneo yote yaliyokuwa na changamoto ya umeme ikiwa ni
pamoja na umeme kutokukatikakatika na watapata umeme wa uhakika.
“Niwaombe sana
Wananchi mchangamkie fursa wewe kama unafuga tumia umeme kama unalima
tumia umeme kwavile ninyi ni wafugaji wekeni umeme hadi kwenye mazizi
kwa ajili ya usalama wa wanyama wenu,”amesema.
Vilevile,amesema
Serikali italipa fidia kwa wote waliotoa maeneo yao kwa ajili ya ujenzi
wa kituo cha kupooza umeme ambapo ekari 130 zitalipwa na jumla ya
shilingi milioni 63 zimetengwa kulipa fidia.
“Ukigushwa utalipwa
inategemea eneo lako lina nini na shughuli za ujenzi zinaanza kuanzia
tarehe 1 mwezi wa 9 ni matarajio yetu mwakani muda kama huu kituo
kitakuwa kimekamlika gharama ni bilioni 41.2,”amesema.
Kuhusiana na
upatikanaji wa umeme katika vitongozi,Wilayani Kongwa,Waziri Kalemani
amesema ameenda na Mkandarasi na Jumatatu ya wiki ijayo umeme utaanza
kuwaka.
“Napenda nitamke
kwamba nimekuja na Mkandarasi huyu hapa sijaja mikono mitupu na Meneja
kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo maana amepewa vitongoji vyote vikiwemo
vitongoji vya Machenjeni hapa Ugogoni na hapa mna vitongoji
vinne,Chungu,Tandika A,Tandika B na Chandama, kuanzia Jumatatu mnaanza
kuwasha umeme na tutaweka umeme kwenye vitongoji vyetu,”amesisitiza
Dkt.Kalemani
Aidha Dkt. Kalemani
amemtaka mkandarasi kuziwekea umeme nyumba zote bila kujali uzuri wa
nyumba huku akiwataka wananchi kulipa shilingi 27 kama Serikali
ilivyoelekeza.
“Ombi langu aanze
kuweka nyaya msijali kwamba ubaya wa nyumba mkandarasi wewe peleka umeme
usiruke nyumba hata moja bei inaelewa ni 27,000 hamuwezi kushindwa
wenyeviti simamieni hili tuna Mheshimiwa Spika kaishaleta fedha za
kutosha tuna bilioni 47 kuwaletea umeme kwenye vitongoji
vyote,”amesema.
Amesema katika Jimbo
la Kongwa wamebakisha vijiji vinne katika vijiji 87 ambavyo bado
havijafikiwa ambapo amedai baada ya kumaliza katika vijiji watahamia
katika vitongoji.
Kwa upande
wake,Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge,Job Ndugai amesema
wakazi wa Jimbo la Kongwa wamekuwa wakilalamika kuhusu umeme kukatika
mara kwa mara.
“Mmekuwa mkilalamika
sana kwenye mitandao yenu umeme ukikatika tu watu wa Kibaingwa tayari
hata watoto wadogo wanajua jinsi Tanesco ilivyomaarufu yaani umeme
ukikatika tu utasikia Tanesco, hata kitoto cha miaka miwili kinajua
Tanesco kwanza kabla ya shirika lolote.
Spika Ndugai amesema lazima Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liondolewe katika sifa hiyo ambayo sio nzuri.
Naye,Kaimu Meneja wa
Tanesco Mkoa wa Dodoma,Mhandisi Donasiano Shamba amesema ujenzi wa
kituo cha Gridi cha 2x40MVA ,220 -33Kv Narco ambacho kitahusisha ujenzi
wa laini ya msongo wa Kilovolti 220 kutoka Zuzu mpaka Narco Kongwa
kwenye kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wenye urefu wa km 122.
Amesema Tanesco
wameishapata eneo lenye ukubwa ekari 130 ambapo zoezi la uthaminishaji
kwa ajili ya fidia ya ardhi na mali limekamilika ambapo wananchi 38
watafidiwa kupisha eneo hilo la mradi.