Waziri
wa Elimu Sayansi na Taknolojia Mhe Joyce Ndalichako akizungumza akiwa
katika eneo la Kibaigwa, Kongwa Dodoma wakati akihitimisha ziara yake ya
kukagua miundombinu ya shule katika Wilaya ya Kongwa.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kongwa Mhe Job Ndugai akizungumza mara baada ya kumalizika kwa
ziara ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe Profesa Joyce
Ndalichako alipofanya ziara ya kukagua miondombinu ya elimu katika
Wilaya ya Kongwa.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Kibaigwa Mwalimu Jema Kihwelo akizungumza mara
baada ya kumalizika kwa ziara ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Mhe Profesa Joyce Ndalichako alipofanya ziara ya kukagua miondombinu ya
elimu katika Wilaya ya Kongwa.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Taknolojia Mhe Joyce Ndalichako mwenye mavazi ya
njano akisikiliza maelezo kutoka kwa Spika wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kongwa Mhe. Job Ndugai wakati
wa ziara ya kukagua miundombinu ya elimu katika Wilaya hiyo.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Taknolojia Mhe Joyce Ndalichako akiagana na Mkuu wa
Shule ya Sekondari Kibaigwa Jamila Kihwelo mara baada ya kumaliza ziara
ya kutembelea Shule hiyo.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Taknolojia Mhe Joyce Ndalichako akizungumza na
wanafunzi wa shule ya Sekondari Ibwaga alipotembelea shule hiyo katika
ziara ya kukagua miondombinu ya elimu katika Wilaya hiyo.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Taknolojia Mhe Joyce Ndalichako akiwa katika picha
ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Ibwaga alipotembelea shule
hiyo katika ziara ya kukagua miondombinu ya elimu katika Wilaya hiyo.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali
ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha ufundi stadi cha Henan cha
nchini China wanatarajia kuanza kujenga chuo cha ufundi stadi
kitakachokuwa kikizalisha wataalamu wa Kilimo na Ufugaji Wilayani Kongwa
Mkoani Dodoma.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa
Joyce Ndalichako wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya elimu
katika Wilaya hiyo ambapo amesema chuo hicho ni kupanua wigo wa
wataalamu hapa nchini.
“Tupo
katika mchakato wa kujenga chuo hicho tukishirikiana na wenzetu wa chuo
cha Henan China tunasubiri tu mchakato wa fedha ili chuo kianze
kujengwa hapa Kongwa” amesema Waziri Ndalichako.
Amesema
Chuo hicho cha China kimeonesha kinalengo la kushirikiana na Tanzania
katika kuinua sekta ya kilimo na mifugo hapa nchini wakishirikiana na
Mamlaka ya elimu ya mafunzo na ufundi stadi VETA kutoa mafunzo hayo.
Wakati
huo huo Waziri Profesa Ndalichako amebainisha kuwa katika kukabiliana
na tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa Serikali kupitia mradi wa
kuimarisha shule za Sekondari wamepanga kujenga shule elfu moja (1000)
katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Amesema
mara kwa mara katika kipindi kama hiki Serikali huwa bize kukabiliana
na uhaba wa vyumba vya madarasa lakini kuanzia mwakani watajenga idadi
hiyo ya shule za Sekondari kuepusha ushumbufu huo ambao hutokea mara kwa
mara katika kipindi hiki.
“Kila
mwaka katika kipindi kama hiki tunakimbizana mpaka tunazuia likizo kwa
Wakurugenzi wa Halmashauri yote ni kuhakikisha watoto wanaingia
madarasani hii tunataka tuikomeshe kabisa” Amesema Prof. Ndalichako.
Pia
ameiagiza Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA kwenda kumalizia mradi wa
ujenzi wa Hosteli za wasichana katika shule ya Sekondari Kibaigwa mradi
ambao waliuanza bila kuumalizia wakati wa kipindi cha uongozi wa nyuma
wa mamlaka hiyo.
Aidha
amesema Serikali itafanya kila jitihada ili kuboresha miondombinu ya
elimu katika Wilaya ya Kongwa sambamba na ujenzi wa shule mpya eneo la
Kibaigwa ili kuepusha msongamano katika wa wanafunzi katika shule hiyo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt Pancras Bujulu akifafanua
kuhusu mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA kipya amesema andiko la mradi
limekamilika na wana subiri taratibu za ujenzi zitaanza mapema baada ya
kukamilika kwa taratibu za serikali.
Nae
Mbunge wa jimbo la Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai
ameshukuru serikali kwa kujenga vyuo vya VETA katika Wilaya hiyo kwani
kwa mda mrefu Wilaya ya Kongwa iliachwa nyuma katika miradi kama hiyo na
kubainisha kuwa wananchi wanafuraha sana ujio wa Chuo cha VETA ambacho
kipo mbioni kukamilika.
Amesema
kuna vijana wengi wanamaliza kidato cha nne katika Wilaya hiyo lakini
walikuwa hawana pa kwenda lakini ujio wa vyuo hivyo utasaidia kutafuta
ujuzi katika vyuo hivyo vinavyojengwa na Serikali.
Katika
ziara hiyo Waziri Profesa Ndalichako amekagua ujenzi wa ofisi za
mdhibiti ubora wa elimu Wilaya ya Kongwa, ujenzi wa chuo cha ufundi
stadi VETA, Shule ya Sekondari Ibwaga na Shule ya Sekondari Kibaigwa.