Serikali yajipanga kutumia filamu kutangaza vivutio vya utalii kimataifa

Na Anitha Jonas – WHUSM,Dar es Salaam.

Viongozi
wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Wizara ya Maliasili
na Utalii wapanga mkakati wa kutumia sekta ya filamu kuwavutia
watengenezaji wa fila

mu kutoka nje kutumia vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Kikao
cha kupanga mkakati huo kimefanyika leo jijini  Dar es Salaam baina ya
wizara hizo ambapo walijadili namna ya kuboresha mazingira ya katika
utoaji wa huduma za waandaji wa filamu kutoka nje ya nchi na kuwavutia
kuja kwa wingi kutumia vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini
kufanya kazi zao.
Akizungumza
katika kikao hicho Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo alisema katika kudumisha mahusiano ya wizara hizo mbili
ambazo zinamwingiliano kutokana na majukumu yake wizara  itaangalia
maslahi mapana ya usalama wa taifa katika kuboresha mazingira ya
uandaaji wa filamu za wadau kutoka nje ya nchi.
“Tumeunda
timu kutoka pande zote mbili ambayo itaenda kuangalia  namna ya
kuboresha mazingira yatakayowavutia waandaji  wa filamu na makala kutoka
nje ya nchi kuja kwa wingi zaidi kufanya kazi zao katika vivutio vyetu,
na watakapomaliza  kazi hiyo wataleta ushauri wao, lengo ni kuhakikisha
nchi inafanikiwa kukuza uchumi,’’ alisema Dkt.Possi.

Pamoja
na hayo Dkt.Possi alisema  kuwa katika kikao hicho walijadili  kuweka
msisitizo pia kuhusu kuhakikisha utoaji wa vibali kwa waandaji wa flamu
za nje unakuwa wa haraka na suala hilo limezingatiwa kwa maslahi ya
Taifa .
Kwa
upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.Adolf Mkenda
alisema nchi inavivutio vingi vizuri na baadhi ni vipya hivyo kwa
kutumia sekta ya filamu inaweza kutangaza vivutio hivyo kwa wingi pasipo
gharama kwani gharama ya kutangaza  vivutio ni kubwa.
“Tunaangalia
namna yakukuza utalii kupitia filamu sababu ni moja ya njia rahisi ya
kutangaza vivutio vya utalii  ni filamu,mfano wa Filamu ya ‘Serengeti 
Shall Never Die’ ilifanya vizuri katika kutangaza mbuga ya Serengeti 
pia ilisaidia  kuongeza idadi ya  watalii katika mbuga hiyo, hivyo
tumeona tuangalie namna ya kuboresha mazingira ya kuwavutia waandaaji
hao wa filamu kuja kufanya kazi zao katika vivutio vyetu kama
Katavi,Gombe,Burigi,Rubondo na vinginevyo,’’alisema Prof.Mkenda.
Aidha,
Katibu Mkuu huyo wa  Wizara ya Maliasili na Utalii aliendelea kusema
kwa sasa vivutio vinavyofanya vizuri katika utalii ni Serengeti,
Ngorongoro ,Kilimanjaro,Manyara , Tarangire na Mikumi  na Tanzania
inavivutio vingi sana hivyo tukitumia fursa ya waandaji wa filamu wa nje
ya nchi itasaidia kuongeza utalii wa vivutio ambavyo bado havijapata
umaarufu.
Halikadhalika
nae Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo alitoa ombi kwa
Wizara ya Maliasili na Utalii  kusaidia kutoa ufadhili wa masomo kwa
wataalamu wa uandaaji wa kazi za filamu nchini kwani kwa sasa kuna 
upungufu  wataalam hao na hii ni changamoto kwa waandaji  wa filamu hizo
wanapokuja nchini na kuhitaji wataalamu hao kutoka nchini.
“Katika 
kuboresha  sekta ya uandaaji wa filamu za kisasa na zenye ubora 
ningeiomba    Wizara ya  Maliasili na Utalii kutoa ufadhiili wa masomo 
ya uandaaji wa kazi za filamu kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) 
kwani kutasaidia kuboresha  vipindi vya kutangaza  vivutio vilivyopo
nchini kupitia Safari Chaneli  ambayo ni chaneli ya kutangaza
utalii”alisema Bibi.Fisoo.
Hatahivyo
nae Kaimu Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho
Kilonzo alisema ofisi yake imeandaa kikao na wadau wanaleta
watengenezaji wa filamu kutoka nje ya nchi  kwa lengo la kuzungumza nao
na kufahamu  ni changamoto gani wanazoziona katika kuwavutia
watengenezaji hao wa filamu kuja kufanya kazi nchini nini kifanyike ili
kuboresha na kufikia malengo ya kutangaza utalii wa vivutio vilivyopo
nchini.