Serikali yakabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi 98,048,000 kwa vikundi vya ujasiriamali wa mazao ya misitu handeni

 

Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa nne kulia) na Balozi
wa  Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan (wa tatu kulia) wakikabidhi
mavazi na buti kwa kikundi cha wajasiriamali cha Uhunzi wa Majiko
Sanifu katika hafla fupi ya kukabidhivifaa vya kuongeza mnyororo wa
thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo
Wilayani Handeni, Tanga.

Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa pili kulia) na Balozi
wa  Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan (wa kwanza kulia)
wakikabidhi mojawapo ya mzinga wa nyuki kati ya mizinga 529 kwa kikundi
cha wajasiriamali cha ufugaji nyuki katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa
vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali
wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga.

Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akihutubia wananchi
katika hafla fupi ya kukabidhivifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa
mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani
Handeni, Tanga.

Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa sita kulia) na Balozi
wa  Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan (wa tano kulia)
wakikabidhi mashine ya kuchakata mbao kwa kikundi cha wajasiriamali cha
uselemala katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa
thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo
Wilayani Handeni, Tanga. Wengine ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
ambaye ni Mkuu wa Wilaa ya Handeni, Mhe. Siriel Mchemba(wa nne kulia).

Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa kwanza kushoto) na
Balozi wa  Finland nchini Tanzania, Mhe. Riita Swan (wa pili kushoto)
wakikabidhi mashine ya kufua umeme kwa kikundi cha wajasiriamali cha
uselemala katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa
thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo
Wilayani Handeni, Tanga. Anayeshuhudia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga ambaye ni Mkuu wa Wilaa ya Handeni, Mhe. Siriel Mchemba(katikati).

Baadhi ya
wananchi wa vijiji vya Wilaya ya Handeni wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akihutubia katika
hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao
ya misitu kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni,
Tanga.

Mkurugenzi wa
Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Ezekiel Mwakalukwa
akitoa maelezo kuhusu uanzishwaji wa mradi wa kuongeza mnyororo wa
thamani wa mazao ya misitu (FORVAC) katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa
vya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali
wadogo iliyofanyika leo Wilayani Handeni, Tanga.

**************************

Na Happiness Shayo-Handeni

Serikali kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii imekabidhi vifaa vya kuongeza mnyororo wa thamani wa
mazao ya misitu kwa vikundi 20 vya wajasiriamali vinavyojihusisha na
ufugaji nyuki, seremala, uhunzi wa majiko banifu kutoka vijiji vya
Mazingara, Kitumbi, Gole, Kwamsundi na Kwedikabu Wilayani Handeni Mkoani
Tanga.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa hafla fupi ya
makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya
ya Handeni.

Mhe. Masanja amesema kuwa makabidhiano hayo ni mwendelezo wa awamu za ugawaji vifaa kwa wanavijiji ili kuinua uchumi wao.

 “Awamu ya kwanza ilifanyika
mwezi Machi, 2021 kwa wananchi wa Wilaya ya Songea Mjini, Namtumbo na
Ruangwa ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
(Mb) alikabidhi mashine tatu za kisasa za kuchakata magogo” amesema Mhe.
Masanja.

Amefafanua kuwa vifaa hivyo
vyenye gharama ya shilingi 98,048,000 ni sehemu ya utekelezaji wa mradi
mkubwa wa kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu (FORVAC) 
ambao pamoja na mambo mengine unaangalia namna bora ya kutumia mazao ya
misitu katika hali ya uendelevu.

Aidha, amewataka wajasiriamali
hao kuhakikisha wanatumia vizuri vifaa walivyokabidhiwa  ili viweze
kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuongeza mapato kwa wananchi.

Naye, Balozi wa Finland nchini
Tanzania, Mhe. Riita Swan amesema mradi wa FORVAC nchini Tanzania
ulianza mwaka 2018 ukiwa ni moja ya miradi mikubwa inayosaidia kukuza
ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Finland.

Amesema lengo la mradi huo ni
kuongeza mapato ya kiuchumi, kijamii na kimazingira kiutokana na misitu
inayopatikana nchini Tanzania.

Balozi Swan ametaja mikoa ambayo mradi huo umekuwa ukitekelezwa kuwa ni Tanga, Ruvuma, Lindi na Dodoma .

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Misitu na Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel
Mwakalukwa amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii ilianzisha mradi
wa FORVAC kwa lengo la kusaidia wananchi kuanzisha na kumiliki misitu ya
vijiji kwa mujibu wa sheria.

Ameongeza kuwa baada ya
wananchi hao kumiliki misitu hiyo, watumie fursa hiyo kuvuna rasilimali
iliyopo kwa njia endelevu ili kukuza uchumi wao.

Hafla ya ugawaji vifaa vya
kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu kwa wajasiriamali wadogo
ilihudhuriwa na Viongozi kutoka Mkoa wa Tanga, Viongozi na Watendaji
kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Viongozi na Watendaji kutoka
FORVAC na wanavijiji wa Wilaya ya Handeni