Shambulio la al-shabab lilivyoathiri usalama eneo la lamu

Al Shabab wamefanya mashambulizi kadhaa ya kikatili Afrika Mashariki
Al Shabab wamefanya mashambulizi kadhaa ya kikatili Afrika Mashariki


Hali ya wasi wasi imetanda katika jimbo la Lamu pwani ya Kenya kutokana na mfululizo wa mashambulio ya kigaidi yaliyolenga kambi ya kijeshi inayotumiwa na majeshi ya Kenya na Marekani.

Jeshi la jeshi la Kenya, KDF limethibitisha wanajeshi watatu wa Marekani na wajenzi wawili wa ulinzi wameuawa katika shambulio la siku ya Jumapili katika eneo la Manda bay.

Jeshi la Kenya limethibitisha vifo hivyo na kusema kuwa Wamarekani wengine wawili wafanyikazi wa kitengo cha ulinzi katika jeshi la Marekani walijeruhiwa katika shambulio hilo lililotokea karibu na mpaka wa Somalia.

 
Watu watatu wauwawa katika shambulio la kigaidi Kenya

Jeshi hilo pia limeelezea kuwa wanamgambo wanne wa Al-shabab waliuawa katika kambi ya Simba iliyoko eneo la Hindi Magogoni pembezoni mwa kisiwa hicho cha kitalii Lamu.

Marekani kwa upande wao wamepuuza shambulio hilo na kudai lilidhibitiwa vilivyo. Image caption Uwanja wa ndege wa Manda, uliopo Lamu 

 
Mashambulizi hayo yamesababisha madhara kiasi gani?

Uwanja wa ndege wa Manda, uliopo Lamu
Uwanja wa ndege wa Manda, uliopo Lamu

Ndege nne za kijeshi mbili za Kenya na zingine mbili za Marekani ziliaharibiwa vibaya katika tukio hilo.

Hali hiyo iliwatia hofu wakaazi wa kisiwa cha Lamu, mmoja wao akiwa mama ambaye hakutaka kutajwa jina kutokana na sababu za kiusala aliiambia BBC:

”Nilisikia sauti ya risasi ni kamuamsha bwanangu… na ndio sasa marisasi yalikuwa yanazidi, ikabidi ni toke niingie mvungu mwa kitanda manake risasi zilikuwa zinalia juu ya paa la nyumba, nikaenda chumba cha watoto cha kulala nikawapta watoto wanalia na ndipo baba yao akanza kuwatuliza”

Anasema ”Risasi ziliendelea kulia hivyo hivyo sasa hakuna kutoka, hakuna kuenda mahali popote kwa nyumba juu unaona moto tu”.

Shambulio hilo la kambi ya kijeshi limetokea siku tatu baada ya shambulizi lengine lililolenga mabasi ya matatu ya abiria yaliyokuwa yamebeba abiria kutoka Mombasa kuelekea Lamu siku ya Alhamisi ambapo watu wanne walipoteza maisha yao. Image caption Mji wa Lamu, kusini mashariki mwa Kenya

Wakaazi waelezea hofu yao

Mji wa Lamu, kusini mashariki mwa Kenya
Mji wa Lamu, kusini mashariki mwa Kenya

Wakati vyombo vya usalama nchini Kenya vikiendelea kudhibiti hali na kutoa usalama kwa wananch wakaazi wa eneo hilo la Lamu wanahofia hali yao ya usalama hasa kufuatia kuripotiwa kwa mashambulizi mawili ya kigaidi

”Haya matatizo ambayo yametokea kuanzia juzi magari kupigwa na jana maeno karibu na uwanja wa ndege kushambuliwa wakati huu ambao shule zinafunguliwa inatutua hofu” alisema Misbaa Aboubakar ambaye ni mkaazi na mzazi ambaye mtoto wake anafaa kurejea shuleni.

”Twataka tuwapeleke shule…Hatujaelewa mpapa saa hii wametupangia nini juzi baada ya masuala ya juzi kupigwa gari na jana kupigwa uwanja wa ndege” alisema Bwana Aboubakar.

Anataka serikali iwabainishie wakaazi wa Lamu mkakati wa kiusalama ili kuwaondolea hofu kuhusu masuala ya usafiri” alisema Bw. Aboubakar.

Wakati ambapo hali ya usalama ikiendelea kukumbwa na changamoto katika eneo hilo huenda sekta ya utalii ambayo ni kitega uchumi wa Lamu ukaathirika. Image caption Manda ni sehemu ambayo jeshi la Marekani utumia kutoa mafunzo ya kijeshi na kikosi kinachotoa usaidizi wa kukabiliana na ugaidi Afrika Mashariki.

 
Manda ni sehemu ambayo jeshi la Marekani utumia kutoa mafunzo ya kijeshi na kikosi kinachotoa usaidizi wa kukabiliana na ugaidi Afrika Mashariki
Manda ni sehemu ambayo jeshi la
Marekani utumia kutoa mafunzo ya kijeshi na kikosi kinachotoa usaidizi
wa kukabiliana na ugaidi Afrika Mashariki
 
Al Shabaab walikuwa wanajaribu kuelekea kambi ya karibu inayotumiwa na Marekani na jeshi la Kenya.

Wakazi wa eneo hilo waliripoti kuwa walikuwa walisikia milipuko na baadae milio ya risasi.

Moshi mzito ulionekana katika eneo la tukio.

Uwanja wa ndege wa Lamu ulifungwa kwa muda lakini taarifa kutoka mamlaka ya usafiri wa ndege nchini Kenya KCAA, imetangaza kurejea tena kwa shughuli za usafiri.

Al-Shabab walidai kuwa kuna vifo vingi na majeruhi wa vikosi vya Marekani na wanajeshi wa Kenya wapo.

Lakini Marekani kwa upande wao wamepuuza shambulio hilo na kudai lilidhibitiwa vilivyo.

Christopher Karns, Msemaji wa kitengo cha Jeshi la Marekani Afrika amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa huo ni uzushi wa kukuza mambo.

Aidha hakufafanua zaidi taarifa hizo, AP imeripoti.

Kambi hiyo ilikuwa na Wamarekani wapatao 100.

Msemaji wa polisi nchini Kenya Charls Owino amesema kuwa wachunguzi wanapeleleza ikiwa ”tukio la Lamu lina uhusiano wowote na Soleimani, kamanda wa jeshi la Iran aliyeuawa na Marekani nchini Iraq wiki iliyopita.

Ikumbukwe kuwa mwezi Juni 2018, Komando wa Marekani aliuwawa nchini Somalia wakati wa shambulio la al-Shabab.

Marekani ilianza operesheni dhidi ya wanamgambo tangu rais Donald Trump aingie madarakani 2017.

Marekani ilifanya mashambulizi mengi zaidi ya anga nchini Somali mwaka 2019 zaidi ya miaka ya nyuma.

Hali ya kiusalama katika fukwe za Manda ni imara.

Na wiki iliyopita kundi hilohilo la kigaidi lilihusika na shambulio lililouwa zaidi ya watu 80 huko Mogadishu.