Shirika la cowoce lashirikiana na wananchi ujenzi wa choo shule ya msingi mapinduzi b mjini shinyanga

 

TAZAMA VIDEO  HAPO JUU

Na Mapuli Kitina
Misalaba

Kamati maalum ya ujenzi
wa  Choo katika Shule ya Msingi Mapinduzi
B, kwa kushirikiana na wazazi,  leo
imezindua rasmi ujenzi wa matundu matatu ya vyoo  na chumba maalum kwa ajili ya wasichana  katika shule hiyo iliyopo katika  Manispaa ya Shinyanga.

Katika taarifa yake
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mwalimu James Msimbang’ombe amesema tayari maandalizi
ya awali yamefanyika na ujenzi umeanza kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana
na shirika la COWOCE.

Mwenyekiti wa mtaa huo kata ya Ngokolo Bwana Chief Thomas Ng’ombe amewasisitiza wananchi kushiriki vema kwenye ujenzi
huo ili kupunguza changamoto ya Vyoo katika shule ya Mapinduzi B.

Akizungumza mratibu wa
ujenzi huo kutoka shirika la Companion of Women and Children Empowerment
(COWOCE) Bi. Grace Moses amesema shirika hilo linatekeleza mradi wa hisani kwa
jamii ambapo amewaomba wananchi na wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi hizo
ikiwemo kushiriki katika shughuli ya ujenzi huo.

“Katika
mazingira haya ugonjwa wowote ule ukilipuka watoto wetu watakuwa kwenye ile
hali ya hatari zaidi lakini leo tunazindua mradi wetu huu wa hisani kwa jamii
niwaombe wananchi tujitoe, kwa mioyo yetu yote tujitoa kwa nguvu zetu zote
tukisema kwamba tunajitaji nguvu kazi wananchi niwaombe kweli nguvu kazi
ionekane siku hizi mpaka wanawake wanabeba Zege kwahiyo jamani tujitahidi
tushirikiane tushikamane hili suala linahitaji nguvu ya pamoja”.amesema Grace

Baadhi ya wananchi
waliojitokeza leo kwenye uzinduzi wa ujenzi huo wamelishukuru shirika la COWOCE
huku wakiahidi kushiriki kikamilifu kwenye shughuli hiyo ya ujenzi.

Kwa upande wake mkuu wa
shule ya msingi Mapinduzi B, Mwalimu Japhet Jasson ameeleza kuwa pamoja na
ujenzi wa matundu hayo ya Choo, bado changamoto ni kubwa kwani matundu ya vyoo
yanayohitajika ni 50, na sasa yaliyopo ni 02.

“Nitoe
shukurani za dhati kwa shirika la COWOCE, kupitia Mkurugenzi wa Manispaa ya
Shinyanga kwa kutoa kibali kwa shirika hili kuendelea na utaratibu huu na mimi
mkuu wa shule nitaendelea kuwapa ushirikiano”.

“Changamoto
hii ya matundu ya Vyoo niya muda mrefu mimi nimehamishiwa hapa nikaikuta ambapo
wanafunzi waliopo kwa sasa ni 1089, watoto wa kiume wanahitaji matundu ya Vyoo
22 na watoto wa kike wanahitaji matundu ya Vyoo 28 ambayo jumla ni matundu 50,
na mpaka sasa hivi ninavyoongea matundu yaliyopo ni mawili tu ya wasichana nayo
yalikuwa ya walimu baada ya kuona kuna uhaba wa matundu ya Vyoo walimu wakawa
wamewapatia wanafunzi wa kike kwahiyo watoto wa kiume mpaka sasa hivi hawana
hata tundu moja la Choo wenyewe wanajisaidia haja zao pembeni”.
Amesema Mwalimu
Japhet

Ujenzi wa matundu
matatu ya Vyoo
  na chumba maalum kwa
ajili ya wasichana
  katika shule ya
msingi Mapinduzi B kata ya Ngokolo  Manispaa ya Shinyanga unatarajiwa kukamilika Mwezi Julai
Mwaka huu 2024.

Mwenyekiti wa kamati
maalum ya ujenzi wa Choo katika shule ya msingi Mapinduzi B,  Mwalimu James Msimbang’ombe akipokea michango
kwa wananchi walioguswa kujitolea ili kufanikisha ujenzi huo.