Shirika la nancy foundation na ubongo learing kwa kushirikiana na serikali yakutana na watendaji ngazi ya kata na mitaa shinyanga wapewa maelekezo muhimu.

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Mashirika mawili
yasiyokuwa ya kiserikali Mkoani Shinyanga Nancy Foundation na Ubongo learing
kwa kushirikiana na serikali yamekutana na watendaji  mbalimbali ngazi ya kata na Mitaa kwa lengo la
kujadili namna bora ya kutatua changamoto ya watoto wanaoishi mitaani.

Kikao hicho kimefanyika
leo April 18, 2023 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika Hospitali ya Mkoa wa
Shinyanga na  kuhudhuriwa na maafisa
watendaji wa kata, wenyeviti wa serikali za mitaa, pamoja na maafisa wa jeshi
la polisi ngazi ya kata katika Manispaa ya shinyanga

Akizungumza katika kikao
hicho Mkurugenzi wa Shirika la Nancy Foundation Ezra Manjerenga pamoja na mambo mengine ameeleza malengo ya kikao hicho
kuwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kuwaondoa  watoto kuishi kwenye mazingira hatarishi.

Kwa upande wake afisa
ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elizabeth Mweyo pamoja na maelekezo mbalimbali amewataka wenyeviti
wa mitaa  kushirikiana ili kuwabaini
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

“Majukumu
yenu ni kuhakikisha mnawafahamu watoto na kuzibaini Familia zao, mnatakiwa kuwa
na takwimu sahihi za watoto wenye changamoto hiyo, mnatakiwa kusaidizana na
maafisa ustawi wa jamii pamoja na viongozi na wadau wengine katika kutatua
tatizo hili lakini mnatakiwa kuwa na mipango yenu ya kumaliza tatizo la watoto
wa mtaani na mnatakiwa kutoa taarifa kwa viongozi wa ngazi za juu pale
mnapokutana na changamoto lakini pia kutoa taarifa kwa wadau wa shirika hili,
mnatakiwa kufanya uhamasishaji kwenye jamii hasa mnapokuwa na mikutano yenu ya
hadhara suala la malezi bora kwa watoto liwe ni kipaumbele ili wazazi wajue
hali halisi ya changamoto hii lakini pia mnatakiwa kuweka makubaliano ya pamoja
na wazazi juu ya watoto wao ikiwa ni pamoja na kuzingatia umri wa watoto
kuajiriwa”.
Amesema Afisa ustawi wa jamii Elizabeth
Mweyo

Nao baadhi ya wenyeviti
wa mitaa kutoka kwenye kata mbalimbali ikiwemo kata ya Ndala, Kitangili,
Chamaguha pamoja na kata ya mjini wamelipongeza shirika la Nancy Foundation kwa
ubunifu huo huku wakiahidi kutoa ushirikiano kwa serikali pamoja na mashirika
hayo katika utekelezaji wa mradi huo.

Mashirika hayo mawili
Nancy Foundation na Ubongo learing yanatekeleza mradi wa Miezi mitatu unaolenga
kupunguza au kumaliza kabisa watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika
Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Shirika la
Nancy Foundation Ezra Manjerenga akizungumza leo April 18,2023 katika kikao cha
pamoja na watendaji mbalimbali ngazi ya kata ya mitaa Manispaa ya Shinyanga

Mkurugenzi wa Shirika la
Nancy Foundation Ezra Manjerenga akizungumza leo April 18,2023 katika kikao cha
pamoja na watendaji mbalimbali ngazi ya kata ya mitaa Manispaa ya Shinyanga

Afisa ustawi wa jamii
Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Bwana Leopald Hamza akizungumza kwenye kikao
hicho leo April 18,2023.

Mtendaji wa kata ya Ndala
Bwana Joshua Masengwa akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Polisi wa kata ya Ndala
Bwana Alimpa Willa akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa mtaa wa
Mitimirefu kata ya Mjini Shinyanga Bwana Nassor Mokh Warioba akizungumza kwenye
kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy Foundation
ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa mtaa wa Banduka
Bwana Pius Mathias akizungumza kwenye kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa
na shirika la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano
Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Mtendaji
talafa ya Shinyanga mjini Bwana Mathias Masalu
akizungumza
kwenye kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy
Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa
Shinyanga.

 

Afisa ustawi wa jamii wa
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Elizabeth
Mweyo
akiwa katika kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika
la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya
Mkoa wa Shinyanga.

Afisa
ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ancila Katero
akiwa katika kikao
hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na shirika la Nancy Foundation ambacho
kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Watendaji wakiwa katika kikao hicho leo April 18,2023 kilichoratibiwa na
shirika la Nancy Foundation ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano
Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga.

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa
mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga leo April 18,2023

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa
mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga leo April 18,2023

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa
mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga leo April 18,2023

Polisi wa kata ya Kitangili Alinsp Shaweji
Halahala wa kwanza upande wa kulia, polisi wa kata ya Mjini Shinyanga Alinsp Jane
Mwazembe katikati pamoja na polisi wa kata ya Ndala Alinsp Alikwin Willa kutoka
upande wa kulia wakiwa kwenye kikao leo April 18,2023.

Polisi wa kata ya Kitangili Alinsp Shaweji
Halahala wa kwanza upande wa kulia, polisi wa kata ya Mjini Shinyanga Alinsp Jane
Mwazembe katikati pamoja na polisi wa kata ya Ndala Alinsp Alikwin Willa kutoka
upande wa kulia wakiwa kwenye kikao leo April 18,2023.

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga leo April 18,2023

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga leo April 18,2023

Mratibu wa usambazaji kutoka Ubongo
learning upande wa kulia akiwa katika mazungumza na Afisa ustawi wa jamii
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Lemiflora Nyalaja kwenye kikao leo
April 18,2023.

Mratibu wa usambazaji kutoka Ubongo
learning upande wa kulia akiwa katika mazungumza na Afisa ustawi wa jamii
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Lemiflora Nyalaja kwenye kikao leo
April 18,2023.