Simanzi kifo cha ras kwitega

Na Mwandishi, Wetu

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Sanare na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Dk Anna Mghwira wamesema pengo aliloacha Richard Kwitega ni kubwa na kuwataka madereva kuwa makini barabarani.

Wakizungumza wakati wakitoa salamu kumuaga aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega ambaye alifariki juzi kwa ajali ya gari wamesema kumpoteza kiongozi huyo ni pengo kubwa.

Sanare amesema alifanya kazi na Kwitega alipokuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha na kwamba Marehemu alikuwa mtu mwema Sana.

“Nilifanya naye kazi alikuwa mtu mwema sana, alikuwa msikivu aliweza kuhimili siasa za Arusha,” amesema

Kwa upande wake Dk Mghwira amesema ajali ya Kwitega inatakiwa kutoa funzo kwa madereva kuwa makini barabarani.

Amesema ajali hiyo ingeweza kuepukika kama madereva wangekuwa makini.

“Chanzo Cha Kifo ni ajali ambayo ingeweza kuepukika, leo tumempoteza kiongozi mwema Sana,” Amesema Kwitega alikuwa akielekea Dodoma kuhudhuria vikao vya viongozi wa Mikoa.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Mdori Kijiji cha vilima vitatu Wilayani Babati mkoa Arusha baada ya gari lake kugongana na Basi la Makala lililokuwa linatoka Singida kwenda Arusha.

Ibada ya kumuaga Kwitega amefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha