Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kampeni ya Shujaa wa
Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imewaomba
wakazi wa Mkoa huo kupaza sauti juu ya ukatili kwa kuripoti vitendo hivyo.
Hayo yamebainishwa na
viongozi wa kampeni hiyo kwenye kikao cha kamati tendaji kilicholenga kujadili
mambo mbalimbali ili kufanikisha shughuli za kupinga ukatili.
Akizungumza kwa niaba ya
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, Mwenyekiti idara ya wanawake
Mwinjilisti Ester Emmanuel amewaomba
wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutofumbia macho vitendo vya ukatili badala yake
wanapaswa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika.
Kwa upande wake naibu
katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Edson Sholagi amesema ipo mikakati
mbalimbali ya kufanikisha kampeni hiyo ambapo wanatarajia kufanya ziara ya
kutembelea Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuibua ukatili na
kuimarisha viongozi ngazi ya chini.
Naye katibu wa SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya ametoa shukurani zake kwa kuteuliwa kutumikia
nafasi hiyo huku akiahidi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa taratibu
zilizopo pamoja na kushirikiana na viongozi wengine.
“Nashukuru
sana kwa uteuzi wa Tarehe 24 Mwezi wa sita Mwaka huu 2023 kwanza kabisa nianze
kumshukuru Mwenyekiti wangu ngazi ya Taifa Shujaa Sospeter Bulugu kwa kuniona
na mimi kijana nafaa ambaye naweza kuchapa kazi nikiwa katibu wa Mkoa na mimi
nitanya kazi kwa juhudi ili kuhakikisha tunapunguza au kumaliza kabisa ukatili,
lakini pia nimshukuru waziri mwenye dhamana mama yetu Dkt. Dorothy Gwajima kwa
kutambua mchango wetu sisi vijana”. Amesema Daniel Kapaya
“Lakini
pia nimshukuru Mwenyekiti wangu wa Mkoa wa Shinyanga Madam Kisendi na
waandamizi wengine nikiwa katibu wa SMAUJATA Mkoa nitashirikiana nao kwa karibu
katika kufanya kazi hii kwa sababu tusipokuwa na ushirikiano maana yake
tutashindwa kutokomeza ukatili, niseme tu kuwa nitajitahidi sana kuanzia ngazi
ya Mkoa, Wilaya, kata, matawi mpaka watu wa chini kabisa tutawafikia ili kuibua
ukatili unaoendelea kufanyika”. Amesema Daniel Kapaya
Mwenyekiti wa SMAUJATA
Taifa shujaa Sospeter Bulugu alimteua Bwana Daniel Kapaya kuwa katibu wa SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga tangu Jumamosi Juni 24,2023.
SMAUJATA ni kampeni ya
kupinga ukatili Nchini iliyoanzishwa Mwaka jana chini ya Waziri wa maendeleo ya
jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima kwa kushirikiana
na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Bwana Sospeter
Mosewe Bulugu.
Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya akishukuru kwa kuteuliwa nafasi hayo.