Spika ndugai azindua mradi wa agri thamani foundation unaotoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za sekondari

 

 

Mkurugenzi
wa Taasisi ya ya Agri Thamani Foundation Neema Lugangira (MB) kushoto
akisalimiana na Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (MB)
Job Ndugai wakati wa hafa hiyo


Mhe Balozi wa China, Mhe Wang Ke kushoto akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi Shule ya Sekondari ya Ibwiga iliyopo Wilaya ya Kongwa katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya ya Agri Thamani Foundation Neema Lugangira (MB) ambayo imezindua Mradi wa kutoa Msaada wa Taulo za kike kwa Wanafunzi wa Sekondari wa Kike.

Mkurugenzi wa Taasisi ya ya Agri Thamani Foundation Neema Lugangira (MB) akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mhe Balozi wa China, Mhe Wang Ke akizungumza wakati wa halfa hiyo
Wanafunzi Shule ya Sekondari ya Ibwiga iliyopo Wilaya ya
Kongwa wakiingia kwa shairi kabla ya kuanza makabidhiano hayo

TAASISI ya Agri Thamani Foundation iliyopo chini ya Neema Lugangira (MB) ambaye ni Mkurugenzi  imezindua
Mradi wa kutoa Msaada wa Taulo za kike kwa Wanafunzi wa Sekondari wa
Kike. 

Lengo la awali lilikuwa kufikia watoto wa kike 1,500 lakini sasa
utafikia watoto wa kike 3,000 kutoka Mikoa 6; Dodoma, Tanga, Tabora,
Kigoma, Kagera na Lindi. 


Mradi
huu umezinduliwa kutoka Shule ya Sekondari ya Ibwiga iliyopo Wilaya ya
Kongwa, Mkoa Dodoma. Jumla ya watoto wa kike 95 ambao mwakani 2021
wanaingia mwaka wa mitihani (Kidato cha Pili na Kidato cha Nne)
wamepokea msaada wa Taulo za Kike za kuwatosha kwa kipindi cha mwaka
mzima kila mmoja.
 
Hivyo, Agri Thamani inaamini kwa kufanya hivi watoto
wa kike hawa hawatakosa shule na hatimae itachangia kuongeza ufaulu wao
kwenye mitihani ya mwakani huku wakiwa na afya na usafi binafsi. 

Agri
Thamani pia wametoa box lenye jumla ya packet 100 za taulo za kike kwa
ajili ya kuwepo shuleni kukidhi mahitaji ya dharura ya mtoto wa kike.

Uzinduzi huu umehudhuriwa na Mhe Balozi wa China, Mhe Wang Ke ambao wanashirikiana na Agri Thamani katika Mradi huu.

Katika
Hafla hii ya Uzinduzi, Mhe Neema Lugangira (Mb) aliwasilisha ombi kwa
Mhe Balozi wa China, Mhe Wang Ke la kuanzisha Mradi wa Wanafunzi wa Kike
wanaomaliza Kidato cha Sita kupata Ufadhili wa kwenda kusoma Vyuo Vikuu
vya China kwenye masomo ya Sayansi. 
 
Mhe
Balozi hapa alikubali ombi hilo
na kwa kuanzia mabinti 3 waliomaliza mwaka huu 2020 watachaguliwa
kupata ufadhili huu na watatoka Wilaya ya Kongwa, Dodoma na Wilaya ya
Bukoba Mjini Kagera. Mhe Neema Lugangira ataratibu zoezi hili
kwa kushirikiana na Mamlaka za Wilaya husika.

Wanafunzi
kwa umoja wao wametoa Shukurani kwa Mhe Neema Lugangira (Mb) kwa
kuwajali wanafunzi wa kike. Mmoja wao kwa niaba ya wote atoa Shukurani
hizo mbele ya wageni.

Awali
akizungumza Mgeni rasmi Mhe Mbunge wa Jimbo la Kongwa ambae pia ni Mhe
Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(MB), Mhe Job Ndugai alisema
msaada huo wa taulo utakuwa chachu kwa wanafunzi wa kike kuweza kusoma
bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ile


Alimshukuru
Balozi huyo kwa kukubali ombi la mbunge Neema la kusaidia mabinti hao
huku akieleza msaada huo unaweza kuchukuliwa kama kitu kidogo lakini ni
mkubwa wenye thamani kubwa sana .


“Maana
ni muhimu sana tuwasaidie watoto wa kike lakini nishukuru kwa shule ya
Ibwaga kuchaguliwa kufanyika kwa uzinduzi huo huku akiliomba Shirika la
Agri Thamani kuweka ofisi Kongwe ili jitihada na mashirikiano hayo
yaendelee.

Naye kwa
upande wake Balozi wa China nchini Mhe Wang Ke alihaidi kuendelea
kushirikiana na Shirika la Agri Thamani na wataongeza ufadhili ili mradi
wa Taulo za Kike ufikie mabinti wengi zaidi. huku wakikubali  ombi la
Shirika hilo la Agri Thamani la “Scholarship” za Masomo vyuo vikuu China
 
 Mhe Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Suleiman Serera aliwapokea wageni na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama.