Chadema watoa kauli kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa

Mwenyekiti
wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hawatasusia uchaguzi wa Serikali za
mitaa wa Novemba 24 mwaka huu na amewataka viongozi, wanachama na
Watanzania kuhamasishana kujiandikisha.


Amesema
hayo leo wakati akizungumza na waandishi ambapo ameeleza  uchaguzi huo
ndio unawaleta viongozi wanaokwenda kutatua changamoto za wananchi hivyo
kuacha serikali ifanye uamuzi ni kosa.

“Tunapaswa
kuweka kando tofauti zetu, twendeni kwa wingi tukajiandikishe ili
tushiriki kwenye uchaguzi huu muhimu,” amesema Mbowe

Ameendelea
kwa kusema wananchi kusuasua kwenda kujiandikisha ni matokeo ya kile
alichodai kuwa ni serikali  kuweka msisitizo katika kuwazuia watu wa
upinzani kufanya mikutano ya kisiasa.

“Ni
makosa makubwa na aibu kususia. Kwa muda wa siku tatu zilizoongezwa,
viongozi wote wa kada zote, wahamasishane watoke kwa wingi kwenda
kujiandikisha, hatuna sababu za kususia kwani tutakuwa tumesusia maisha
yetu,” amesisitiza Mbowe


“Tunakwenda kushiriki uchaguzi huu na tutashinda, hatutakuwa woga na
haya ni mapambano ya kisiasa, tutatumia nguvu za umma kuhakikisha
tunashinda uchaguzi huu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *