Taasisi ya flaviana matata foundation yakabidhi mradi wa vyoo vyenye matundu 24 shinyanga, viongozi wataka ufaulu uongezeke kwa wanafunzi.

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Taasisi ya Flaviana
Matata Foundation leo imekabidhi mradi wa vyoo viwili vyenye matundu 24 katika
Shule ya sekeondari Mazinge iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga vyenye
thaman ya shilingi milioni 58 kama hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali.

Akizungumza Meneja miradi
wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation Lineth Masala amesema mradi huo
umelenga kuondoa changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo katika shule hiyo.

Amesema mradi huo umeanza
kutekelezwa Mwezi Machi Mwaka huu 2023 ambapo umekamilika Mwezi Julai 2023 na
kwamba taasisi ya Flaviana Matata Foundation inatekeleza miradi kupitia
ufadhili wa Diamonds do good.

Akizungumza katika hafla
ya kukabidhi vyoo hivyo mkurugenzi wa taasisi ya Flaviana Matata Foundation
amesisitiza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kutunza miundombinu ya mradi huo
ili uweze kudumu na kuendelea kuwanufaisha.

Flaviana Matata ameisihi
jamii kuacha mila potovu ambapo amewaomba wazazi kutimiza wajibu wao katika
malezi bora kwa watoto huku akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze
kutimiza ndoto zao.

“Tunamshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tunaamini hivi
tunavyovifanya kwa kushirikiana na serikali vitaenda kutatua changamoto
zilizopo wazazi mpo walimu na wanafunzi niwaombe tuvunje mila potovu tuwaache
watoto wa kike wasome tuache mimba na ndoa za utotoni hivi vyoo tumejenga kwa
lengo la kutatua changamoto zilizokuwepo”

“Sisi
tumejikita kuhakikisha tunatatua changamoto zinazomkabili mtoto wa kike ili
aweze kupata elimu na kujikwamua kiuchumi na sisi tutaendelea kushirikiana na
ninyi siku zote lakini niwaombe mvitunze ili vije kutumiwe na wadogo zenu
wanaofuata na viongozi mtusaidia kutunza miundombinu lakini pia tutafurahi
kuona matokea ufaulu unaongezeka”.
Amesema Flaviana Matata

Kwa upande wake mgani
rasmi kwenye hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameipongeza
taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kutatua changamoto ya vyoo katika
shule ya sekondari Mazinge ambapo amesisitiza wanafunzi kuongeza juhudi katika
masomo ili kuwatia moyo wadau wa maendeleo wanaowekeza mazingira bora na salama.

“Niipongeze
sana taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa kukabidhi mradi huu leo lakini  Mradi huu ambao umeletwa na taasisi ya Flaviana
Matata Foundation wanafunzi wa shule ya sekondari Mazinge ni wanufaika wa moja
kwa moja tunaamini mazingira haya yatasaidia kuongeza ufaulu darasani hasa kwa
watoto wa kike ambao kipindi cha nyumba mlikuwa mnashindwa kufika shuleni,
niwaombe wanafunzi wote mtumie vyoo hivi kama ilivyokusudiwa ili uweze kuishi
miaka mingi tusiharibu miundombinu”.
amesema DC Samizi

Mkurugenzi wa Manispaa ya
Shinyanga Dkt. Jomaary Satura naye ameipongeza taasisi ya Flaviana Matata
Foundation kwa kuendelea kuisaidia serikali kutatua changamoto zilizopo ambapo
amesema   serikali Manispaa hiyo itaendelea kushirikiana
na wadau wa maendeleo kwa kuruhusu uwekezaji hasa katika sekta ya elimu.

Naye Mkuu wa Shule ya
sekondari Mazinge  Mwalimu James Msimba
amesema vyoo hivyo vitakuwa ni chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na
kwamba ameishukuru taasisi ya Flaviana Matata Foundation huku akiomba kuendelea
kushirikiana katika kutatua changamoto zingine zilizopo.

“Uongozi
na jumuiya ya shule ya sekondari Mazinge tunaishukuru serikali yetu ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi shupavu wa Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa kuweka mazingira salama kwa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali”

“Tunaishukuru
taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa msaada wao wa kutujengea matundu 24
ya vyoo pia kwa msaada wa taulo za kike ambazo walitoa kwa wanafunzi wa kike
135 katika shule yetu Mungu awabariki sana kwa moyo wenu wa majitoleo na upendo”.
amesema
Mwalimu James mkuu wa shule

Baadhi ya wanafunzi wa
shule ya sekondari Mazinge wamesema vyoo hivyo vitawasaidia kuondokana na
changamoto zilizokuwa zinawakabili hasa kwa wanafunzi wa kike.

Taasisi ya Flaviana
Matata Foundation leo Juni mosi,2023 imekabidhi vyoo viwili vyenye matundu 24 ambavyo
vina thaman ya shilingi milioni 58 kama hatua ya kuunga mkono juhudi za
serikali katika Shule ya sekeondari Mazinge iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga

Mkurugenzi wa taasisi ya
Flaviana Matata Foundation, Flaviana Mtata akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi vyoo ya kisasa katika shule ya sekondari Mazinge Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga leo Juni mosi 2023.

Mkurugenzi wa taasisi ya
Flaviana Matata Foundation, Flaviana Mtata akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi vyoo ya kisasa katika shule ya sekondari Mazinge Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga leo Juni mosi 2023.

Mkurugenzi wa taasisi ya
Flaviana Matata Foundation, Flaviana Mtata akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi vyoo ya kisasa katika shule ya sekondari Mazinge Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga leo Juni mosi 2023.

Mgeni rasmi, mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye hafla iliyoratibiwa
na taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kukabidhi mradi wa
matundu ya vyoo leo Juni mosi 2023 katika shule ya sekondari Mazinge Manispaa
ya Shinyanga.

Mgeni rasmi, mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye hafla iliyoratibiwa
na taasisi ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kukabidhi mradi wa
matundu ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 58 katika shule ya sekondari Mazinge Manispaa
ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa taasisi ya
Flaviana Matata Foundation, Flaviana Mtata upande wa kushoto na Mgeni rasmi,
mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi wakiteta jambo kwenye hafla ya
kukabidhi vyoo vya kisasa shule ya sekondari Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Manispaa ya
Shinyanga Dkt. Jomaary Satura akizungumza kwenye hafla iliyoratibiwa na taasisi
ya Flaviana Matata Foundation kwa ajili ya kukabidhi mradi wa matundu ya vyoo
yenye thamani ya shilingi milioni 58 leo katika shule ya sekondari Mazinge.

Meneja miradi wa taasisi
ya Flaviana Matata Foundation Lineth Masala akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi mradi wa matundu ya vyoo leo Juni mosi 2023 katika shule ya sekondari
Mazinge Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Shule ya
sekondari Mazinge  Mwalimu James Msimba
akisoma taarifa ya shule kwa mgeni rasmi katika hafla ya kupokea mradi wa
matundu ya vyoo 24 yenye thamani ya shilingi milioni 58.