Tarehe ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji form uchaguzi serikali za mitaa yatangazwa

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani
Jafo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini
Dodoma wakati akitangaza tarehe ya uchukuaji na urejreshaji form za
kugombea nafasi mbalimbali uchaguzi Serikali za Mitaa


Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo,
ametangaza rasmi kuanza kwa zoezi la kuchukua na kurejesha form za
kugombea nafasi mbalimbali katika ngazi za vijiji, Mitaa, Vitongoji na
wajumbe, kwa ajili ya uchaguzi serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba
24 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi
wa habari leo Ofisini kwake, Jijini Dodoma, Waziri Jafo amesema zoezi
hilo litaanza kesho tarehe 29, Octoba na litahitimishwa tarehe 4
Novemba, 2019, zoezi ambalo litakuwa la siku tisa.
Aidha amesema wenye sifa
ya kuchukua form ni wale wanaotoka katika vyama vyenye usajili wa
kudumu, na kuwataka wale wenye nia ya kuongoza katika serikali za Mitaa
ndio mda mwafaka kwenda kuchukua form za kugombea kupitia vyama vyao.
“Zoezi hili litaanza
rasmi kesho tarehe 29/10 na litahitimishwa siku ya tarehe 4/11, 2019, na
watakao takiwa kugombea ni wale wanaotoka katika vyama vyenye usajili
wa kudumu hapa nchini na wale wenye sifa wajitokeze kwa wingi” amesema
Waziri Jafo.
Aidha amesema maandalizi
yote kwa ajili ya zoezi hilo yamekamilika, na kuwataka watu wote
wazingatie kanuni na taratibu wakati wa zoezi la uchukuaji na urejeshaji
wa form hizo na kuwataka wasimamizi na wasaidizi wao kusimamia
kikamilifu zoezi hilo.
Katika hatua nyingine
amewataka Wakuu wa mikoa na Wilaya ambao ndio wasimamizi wa ulinzi na
usalama kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama unakuwepo katika mda wote
wa zoezi hilo.
Amebainisha kuwa
ameshatoa barua ya ufafanuzi  kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili
wa kudumu kuhusu namna ya uchukuaji na urejeshaji wa form, na amevitaka
vyama vyote vizingatie demokrasia wakati wote wa zoezi hilo.
Pia amesema mnamo Oktoba
22, mwaka huu alitoa maelekezo kuwa viongozi wa vijiji, vitongoji,
Mitaa, na wajumbe wote uongozi wao ulikoma tarehe hiyo na kwamba
shughuri zote zinazohusu ngazi hizo zitafanywa na watendaji wa vijiji,
Kata na Wakurugenzi wa Halmashauri.
Amesema “kuanzia tarehe
hiyo wenyeviti wa Mitaa,vijiji, vitongoji na wajumbe, hawataruhusiwa
kutekeleza majukumu yao yoyote kwenye maeneo yao, badala yake Kama
kutakuwa na Jambo wanapaswa kushirikiana na kuamuliwa na mtendaji wa
Kijiji, Kata na Mkurugenzi wa Halmashauri” amesema