Tbs yafanya msako wa bidhaa ambazo hazikidhi viwango kanda ya ziwa

Wakaguzi
wa TBS kanda ya ziwa wakiwa katika ukaguzi wa kushtukiza katika viwanda
vya kuzalisha mifuko ya sandarusi vilivyopo jijini Mwanza kwa ajili ya
kuangalia uzalishaji pamoja na uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya kupima
maabara kama zimekidhi matakwa ya kiwango husika. 

Mkaguzi wa TBS kanda ya ziwa
Bw.Donald Mkonyi akiangalia ukomo wa matumizi ya bidhaa katika duka la
chakula wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni katika Halmashauri ya
Nyamagana. Wauzaji walisisitizwa kuziondoa sokoni mara moja bidhaa
zinapokwisha muda wake wa matumizi kwani zinahatarisha usalama wa afya
za walaji.




Shirika la Viwango Tanzania TBS
limeendelea na ukaguzi wa bidhaa kanda ya ziwa ambapo imefanya ukaguzi
katika maduka ya chakula pamoja na viwanda vya kuzalisha mifuko ya
sandarusi jijini Mwanza.


Wazalishaji wameshauliwa kuzalisha
bidhaa zilizokidhi viwango ili kuweza kumlinda mteja, wakati huohuo
wauzaji wa bidhaa wametakiwa kuhakikisha wanaziondoa sokoni mara moja
bidhaa zinapokwisha muda wake wa matumizi kwani zinahatarisha usalama wa
afya za walaji.