Tbs yatoa mafunzo kwa wazalishaji, waagizaji na wasambazaji wa vifungashio na mifuko mbadala jijini mwanza

 

Maafisa wa TBS wakitoa mada kuhusu masuala ya kuzingatia katika
uzalishaji wa vifungashio na mifuko mbadala sambamba na utaratibu wa
uthibitishaji ubora wa bidhaa wakati wa mafunzo kwa wazalishaji,
waagizaji, wasambazaji na wauzaji wa vifungashio na mifuko mbadala
yaliyofanyika katika ukumbi wa TMDA Mwanza.

Wazalishaji na wasambazaji wa vifungashio vya plastiki na mifuko
wakifuatilia mafunzo kuhusu masuala ya kuzingatia katika uzalishaji wa
vifungashio na mifuko mbadala sambamba na utaratibu wa uthibitishaji
ubora wa bidhaa yaliyofanyika katika ukumbi wa TMDA Mwanza. 

 NA MWANDISHI WETU

 Shirika
la Viwango Tanzania (TBS) limekutana na wazalishaji, wasambazaji na
Vifungashio vya plastiki na mifuko mbadala kwa ajili ya kujadili ni
namna gani wanaweza kuzingatia matakwa ya viwango ili kulinda mazingira
na mtumiaji wa bidhaa husika. 

 Lengo la semina ni kutoa elimu
kuhusu matakwa ya kiwango husika pamoja na sheria na kanuni za kufuata
wakati wa kuzalisha au kuagiza bidhaa hizo, ili kufanikisha lengo hilo
TBS imeshirikiana na NEMC katika mafunzo hayo. 

Akizungumza baada
ya mafunzo hayo Meneja wa Kanda ya Ziwa (TBS) Bw. Joseph Ismail amesema
kuwa changamoto iliyopo kwa sasa ni uelewa mdogo kuhusu matakwa ya
viwango , sheria na kanuni zinazosimamia ualishaji na uagizaji wa bidhaa
za vifungshio vya plastiki vilivyoruhusia na mifuko mbadala.

 “Kama
huelewi viwango vinataka nini kwa bidhaa husika na pia huelewi sheria
na kanuni zinazotakiwa kufuata kabla ya uzalishaji ama uagizaji wa
bidhaa husika kuna hatari kubwa ya kuzalisha na kuagiza na kuingiza
sokoni bidhaa hafifu jambo litakalo ongeza malalamiko kwa watumiaji wa
bidhaa hizo”. 

 Kwa upende wake Afisa Viwango (TBS) Bw. Johnson
Kiwia amesema kuna waagizaji wameanza kuingiza mifuko mbadala isiyofuata
matakwa ya viwango sokoni hali inayopelekea uwepo wa malalamiko mengi
kutoka kwa watumiaji. 

Ukweli ni kwamba sio wote wanaweza
kushiriki katika sekta hii ya biashara , watumiaji hutegemea sana
wasambazaji ili wawashauri juu ya aina ya ubora wanazozihitaji sokoni na
iwapo wazalishaji sasa wamenza kuingiza sokoni mifuko myepesi ambayo
haifiki GSM 70 kama matakwa ya kiwango yanavyosema hupelekea mtumiaji
kupata bidhaa isiyoendana na mahitaji yake ni hii husababisha uwepo wa
malalamiko juu ya thamani ya Maisha yao na fedha zao. Amesema Bw.
Kiwia. 

 Pia Katibu wa Masoko mkoa wa Mwanza Bw. Kurwijila Makubi
Athumani, amesema kupitia mafunzo hayo wametambua kanuni na taratibu
zinazotakiwa kufuata kabla ya kuzalisha, kuagiza na kusambaza bidhaa za
vifungashio vya plastiki vilivyoruhusiwa pamoja na mifumo mbala na
ameahidi kuendelea kudumisha uhusiano na TBS ili kuisaidia nchi
kuzalisha na kuingiza bidhaa bora na kulinda mazingira na watumiaji.

 Pamoja
na hayo Afisa Masoko (TBS) Bi. Rhoda Mayugu amewakaribisha wadau
mbalimbali wenye maoni na changamoto wanazozipitia kuziwasilisha TBS ili
kuzitatua na kuboresha utoaji huduma.