Mkurugenzi wa Shirika la Viwango
Tanzania (TBS), Dkt.Athumani Ngenya akifungua mafunzo kwa wahariri wa
vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ugezi wa
TBS, Mhandisi Johannes Maganga akieleza utofauti wa Upimaji na Ugezi
katika hafla ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika
leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Maabara ya Kemia Bw.Charles Batakanwa akiwasilisha mada ya
“Uwekaji wa kinasaba katika Mafuta” katika mafunzo kwa wahariri wa
vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini
Dar es Salaam.
Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa
zinazotoka nje ya nchi, Mhandisi Said Mkwawa akiwasilisha mada ya
“Ukaguzi wa Magari yaliyotumika yaliyowasili nchini ” katika mafunzo kwa
wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika
hilo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Bw.Diocles Ntamulyango akidadavua jambo
kwenye mada ya “Ukaguzi wa Magari yaliyotumika yaliyowasili nchini”
katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao
Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Masoko Bi.Gladness Kaseka akiwasilisha mada ya “Majukumu ya TBS” katika
mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu
ya TBS Jijini Dar es Salaam.
Mhariri wa Dar Mpya Media Bw.John
Marwa akichangia jambo katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari
yaliyofanyika leo Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
Mhariri Mkuu wa Times Fm Bi.Tausi
Mboya akichangia jambo katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari
yaliyofanyika leo Makao Makuu yaTBS Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
limewataka waagizaji wa magari nje ya nchi kutokuagiza magari kwa watu
binafsi badala yake watumie makampuni yanayoaminika na kufahamika ili
kuepuka kupata hasara kama gari likiwa halina ubora wa viwango
unaotakiwa.
Akizungumza leo akifungua mafunzo
kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya majukumu ya Shirika hilo
yaliyofanyika Makao Makuu ya TBS leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
mkuu wa TBS, Dkt Athuman Ngenya amesema kuwa uagizaji wa gari kupitia
kampuni inayofahamika ni bora kwa maana tatizo lolote llinalohusu gari
ambalo limegizwa kupitia kampuni hiyo itahusika.
“Kama ikitokea muagizaji wa gari
atakuta kuna hitirafu ya gari basi kampuni aliyoitumia itahusika na
matengenezo na kama muhusika hatatumia njia hiyo basi atakuwa kapata
hasara kwani litakuwa limekosa viwango vinavyotakiwa”. Amesema
Dkt.Ngenya.
Aidha kwa upande wake Meneja wa
Ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi Mhandisi Said Mkwawa
akizungumzia kuhusu ukaguzi wa magari yatokayo nje ya nchi amesema
ukaguzi huo pia umefanikisha kukusanya kiasi cha bilioni 1.5 ambazo hapo
awali wangepata asilimia 30 pekee
“Katika magari 4779 tulioyafanyia
ukaguzi kuanzia mwezi aprili 15 mpaka June 08, asilimia 85 ya changamoto
kubwa imejitokeza kwenye ubovu wa kashata,taa, na magurudumu kuisha
muda wake”. Amesema Mhandisi Mkwawa.