Tcra yaongeza muda wa usajili kwa wananchi wa makambako hadi disemba 6, 2019 desemba sita.

Kampuni za simu wakisajili  Wananchi wa Mji Mdogo wa Makambako laini za simu kwa alama za vidole
Wananchi wakipata huduma ya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mji Mdogo wa Makambako
Kufuatia na kujitokeza kwa wingi kwa wakazi wa Makambako
na viunga vyake vya jirani katika zoezi la kupata namba za vitambulisho
vya taifa na kusajili simu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kushirikiana
na Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA na watoa huduma wote wa
makampuni ya simu wameongeza muda wa zoezi hilo  ambapo  sasa zoezi hilo
utafanyika kwa wiki  nzima kuanzia Desemba  2 hadi 6  2019
 Akizungumzia
 maendeleo ya zoezi hilo linaloratibiwa na TCRA mkuu wa kanda ya Nyanda
za juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema lengo la serikali ni
kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaopata huduma za msingi kwa urahisi
hivyo kuongeza huko kwa siku kunalenga kutekeleza  malengo hayo.
Amesema
huo ni muendelezo wa kampeni ya “Mnada kwa Mnada, Karibu tukuhudumie”
iliyoanzishwa na kuratibiwa na TCRA   na kushirikisha wadau wengine
 inayolenga kutoa elimu ya utumiaji bora na salama wa huduma za
mawasiliano  na kuhamasisha usajili wa laini kwa kutumia namba za
vitambulisho vya taifa.