Tic yaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kuwekeza tanzania

 

 Meneja
wa Kanda ya Mashariki TIC, Bw.Bevin Ngezi akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kutembelea mradi wa Mlimani City na kufanya
mazungumza na uongozi wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) leo
Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mkuu wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) Bw.Pastory Mrosso
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelewa na Meneja
wa Kanda ya Mashariki TIC leo kwenye ofisi yake Jijini Dar es Salaam. Meneja
wa Kanda ya Mashariki TIC, Bw.Bevin Ngezi (katikati) akizungumza jambo
na Mkurugenzi Mkuu wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) Bw.Pastory
Mrosso mara baada ya kutembelea mradi huo leo Jijini Dar es Salaam. Meneja
wa Kanda ya Mashariki TIC, Bw.Bevin Ngezi (Kulia) akimsikiliza
Mkurugenzi Mkuu wa Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) Bw.Pastory
Mrosso mara baada ya kutembelea ofisi za mradi huo leo Jijini Dar es
Salaam.

Meneja wa Kanda ya
Mashariki wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Bevin Ngenzi akiwa
na ujumbe kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania wakiwa katika picha na
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mlimani Holdings Ltd, Bw. Pastory Mrosso ambao
ni wawekezaji wa mradi wa Mliamani city baada ya kikao na ukaguzi wa
mradi huo, leo Aprili 22, 2021 Dar es Salaam.

NA EMMANUEL MBATILO

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
kimewakaribisha wawekezaji kuendelea kuwekeza hapa nchini kwani nchi ipo
salama na Serikali ipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kuweza
kupata mafanikio.

Ameyasema hayo leo Meneja wa Kanda ya
Mashariki TIC, Bw.Bevin Ngezi alipotembelea Mlimani City na kukutana na
muwekezaji wa mradi huo.

Akizungumza baada ya kukutana na
muwekezaji wa Mlimani Holdings limited (Mlimani City), Bw.Ngezi amesema
Tanzania ipo tulivu kisiasa na ina mafanikio makubwa kibiashara ambapo
ni rahisi sana muwekezaji kuwekeza na kuweza kupata mafanikio makubwa.

“Tumeona Mlimani holdings limited
wameweza kuwekeza na kupata mafanikio hivyo tunawatia moyo wawekezaji
wazawa na wawekezaji wengine kuja kuwekeza Tanzania kwa maana Tanzania
kuna watu wema na kwenye mafanikio ha kibiashara”. Amesema Bw.Ngezi.

Aidha Bw.Ngezi amesema kuwa uwekezaji
uliofanywa na Mlimani Holdings Limited umesaidia kutoa ajira kwa
watanzania pamoja na kuinua maisha ya watanzania kwa ujumla.

“Uwekazaji Uliofanywa na Mlimani Holdings
Limited umesaidia kutoa ajira zaidi ya elfu 2 kwa watanzania pia wapo
wanaokuja kufanya biashara na kutoa kwahiyo wapo wengi wamefaidika na
uwepo wa Mlimani City”. Amesema Bw.Ngezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Mlimani Holdings Limited (Mlimani City) Bw.Pastory Mrosso amesema tangu
kuanzishwa kwa mradi huo, TIC imekuwa nyuma ya mafanikio ya Mlimani City
mpaka ulipofikia kwa maana serikali ilikuwa na sehemu ya utekelezaji wa
mradi huo.

“Serikali imejitahidi kwa kila hali
kuhakikisha mradi unatekeleza kwa yale yote muwekezaji aliyokuwa
amekusudia na kuleta manufaa makubwa kwa watanzania”. Amesema Bw.Mrosso.

Pamoja na hayo Bw.Mrosso amesema serikali
inapata mapato kupitia kodi kutoka kwa muwekezaji pamoja na waliowekeza
maduka kwenye mradi huo.