Waandishi wa habari wakifuatilia wakati Karibu wa Itikadi na Uenezi TLP taifa akiongea nao leo jijini Arusha |
Waandishi wa habari wakifuatilia mazungumzo ya viongozi wa TLP waliokuwa wakiongea nao kwenye ukumbi wa hotel ya Golden Rose jijini Arusha leo |
Katibu wa Itikadi na Uenezi taifa wa TLP akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari akielezea mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu mwezi wa kumi Tarehe 25 picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Chama cha Tanzania Labour Party TLP kimeunda timu ya kuzunguka nchi nzima kuzungumzia miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu tano chini ya Dkt.John Magufuli kama kuonyesha Juhudi za kuungamkono kwa vitendo kauli ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Aidha chama hicho kimeendelea kuwapongeza Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Dkt.Agustine Mrema kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Makamu wake bara Bi Dominata Rwechungura na visiwani Husein Juma sanjari na kuhamasisha kukijenga chama na kuhakikisha Mh.Dkt.Magufuli anashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.
Akiongea na vyombo vya habari mkoani Arusha Katibu Mwenezi wa taifa wa chama hicho Godfrey Stephen amesema kuwa baada ya kamati kuu kumpitisha kwa kauli moja mgombea wa CCM Dkt. Magufuli kuwa ndie anafaa kugombea kwa mwaka huu katika uchaguzi mkuu na chama hicho kumuunga mkono mgombea huyo.
Alisema kuwa kupitia kikosi kazi hicho watapita nchi nzima kuelezea na kumnadi mgombea huyo kwa wananchi ili wafahamu utekelezaji wa serikali yake katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ndio maana kwa kauli moja kamati kuu ikaona anafaa kuungwa mkono na chama hicho kwa nafasi ya urais.
Kwa mujibu wa Katibu huyo wa chama hicho ameeleza kuwa chama hicho kimejipanga upya ikiwa ni pamoja na kusimamisha wagombea nchi nzima kwa nafasi ya Ubunge na udiwani kwa kuwa ikumbukwe kuwa TLP ndio chuo cha wagombea.
“Kama unavyojua chama chetu kimezaliwa upya baada ya kufanya uchaguzi wa viongozi na Mwenyekiti wetu kuendelea kuwa Agustine Mrema hivyo sura mpya ya uongozi wa.chama chetu unaakisi mageuzi makubwa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu”
Awali akiongea kwenye Kikao hicho na waandishi wa habari Katibu mkuu wa chama hicho mkoa wa Arusha Kinanzaro Geogrey alieleza kuwa chama hicho mkoa wa Arusha litasimamisha wagombea kwenye majimbo yote sanjari na nafasi za Udiwani.
Alisema kuwa mfano mzuri chama hicho kwa jimbo la Arusha mjini pia kitasimamisha mgombea kwani historia inaonyesha wagombea wote waliotoka TLP ni bora hata huyu mbunge ni zao la chama chetu.
Alisema wapo wanachama wa.vyama.vyengine wanaofanya vizuri wote wametoka ndani ya chama hicho hivyo ndio maana wanajipanga kuona wananzalisha wanasiasa ambao watasaidia nchi kufikia malengo yenye tija kwa nchi yetu.
“Niwatoe hofu maamuzi ya kumpitisha mgombea wa nafasi ya Urais wa chama chetu kuwa ni Dkt.John Magufuli wa CCM yamefanywa na kupewa baraka na mkutano mkuu wa chama chetu na sio maamuzi yake pekee mwenyekiti bali ya wajumbe wote wa mkutano huo”