Tma yatoa tahadhari ya mvua kubwa katika mikoa mitatu

Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania ( TMA) imetoa tahadhali ya mvua kubwa
itakayonyesha katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa
Morogoro leo Jumatano Januari 22, 2020.



TMA
imetoa tahadhali ya upepo mkali na mawimbi makubwa katika mikoa ya
Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja
na Pemba.

Taarifa
ya TMA iliyotolewa jana Jumanne Januari 21,2020 inasema mvua hizo 
zinaweza kuleta athari ikiwamo uharibifu wa miundombinu na mali na
makazi kuzunguukwa na maji.

Athari
zingine zinazoweza kutokea hatari kwa maisha ya watu kutokana na maji
kutiririka kwa kasi, ucheleweshaji wa usafiri na kusimama kwa baadhi ya
shughuli za kiuchumi.

Kwa
upande wa tahadhali ya upepo mkali na mawimbi makubwa TMA imesema
athari zinazoweza kujitokeza katika mikoa hiyo kuathirika kwa shughuli
za uvuvi, ucheleweshaji wa usafiri pamoja na kuanguka kwa majani na
matawi ya miti.