Bunge la seneti marekani laidhinisha mpango wa kumuondoa madarakani rais trump

Baraza
la seneti nchini Marekani limepiga kura kwa misingi ya chama na
kuidhinisha sheria zitakazotumika katika kesi ya kumuondoa madarakani
Rais Donald Trump. 


Baraza
hilo lililo na idadi kubwa ya maseneta wa chama cha Republican
limezikataa juhudi za Wademocrat za kupata ushahidi na kuhakikisha
kwamba mashahidi wanasikilizwa. 

Wakili
mkuu wa Trump katika kesi hiyo amesema kesi ya Wademocrat ni juhudi
zisizo na msingi kutaka kupindua ushindi wa Trump katika uchaguzi wa
mwaka 2016 ingawa mbunge mmoja wa chama cha Democratic amesema kuna
ushahidi wa kutosha kuonyesha makosa ya Trump. 

Baraza
la wawakilishi la bunge la Marekani lilipiga kura ya kumuondoa
madarakani Trump mwezi uliopita kutokana na madai ya matumizi mabaya ya
madaraka na kuzuwia mamlaka ya bunge la Congress kwa kuishinikiza
Ukraine kumchunguza hasimu wake wa kisiasa ambaye ni makamu wa rais wa
zamani Joe Biden wa chama cha Democratic. 

Trump anashikilia hakufanya makosa yoyote.