Ugomvi wa wazazi waelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwaharibu watoto kisaikolojia na kuwashusha kitaaluma

Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe akiongea katika katika maafali ya 11  ya kidato cha nne pamoja na  maafali ya 17 ya darasa la saba yaliofanyika katika viwanja Wa shule hiyo vilivyoko katika kijiji  Olosiva 
Wanafunzi wa kidato cha nne wakicheza wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao
wanafunzi wa chekechea wakicheza ngoma kwa ajili ya kuwaaga kaka zao na dada zao wanaoitimu elimu yao ya msingi pamoja na sekondari
Afisa utawala Wa shuleza Trust st.Patrick schools   Dinna Patick Khanya akiongea katika mahafali hayo
mkurugenzi mkuu wa shule ya  Trust St Patrick  schools Patrick  Thomas Khanya  alisema kuwa jumla ya wanafunzi 76  wamehitimu darasa  la saba ,huku wanafunzi  41 wakihitimu kidato cha nne  tangu kuanzishwa kwa shule hiyo
Wanafunzi wa darasa la saba wakicheza mbale ya mgeni rasmi wakati wakiimba wimbo wa kuwaaga wadogo zao 

Na
Woinde Shizza, APC BLOG, ARUSHA 

Imebainika kuwa 
ugomvi Wa familia majumbani  hususani wazazi unachangia kwa kiasi kikubwa
baadhi ya watoto kushindwa kufanya vizuri
kwenye masomo, na muda mungine kusababisha kufeli  kwa masomo yao
shuleni.


Hayo yamebainishwa
na  Afisa utawala wa shule za Trust st.Patrick schools   Dinna Patick Khanya 
katika maafali ya 11  ya kidato cha nne pamoja na  maafali ya 17 ya darasa la saba yaliofanyika
katika viwanja Wa shule hiyo vilivyoko katika kijiji  Olosiva ndani ya halmashauri ya Arusha
wilayani Arumeru ambapo  alisema kuwa  asilimia kubwa ya wanafunzi
wanaofeli darasani ,ni kutokana na ugomvi  wawazazi majumbami.

Aidha pia amesema kuwa wazazi
wengi wamekuwa hawana tabia ya kukaa na watoto wao na kuongea kuhusiana na
mambo mbalimbali yanayowahusu pamoja na kuwaeleza namna dunia inavyoenda ,
kuwaeleza mambo mabaya yaliopo duniani.

Alisema baadhi matatizo ya ugomvi wa familia
yanachangia kwa kiasi kikubwa kuwaadhiri watoto haswa wawapo masomoni kwani mda
mungine   wanashidwa kuwa makini darasani
kutokana na kuathirika kisaikolojia  
kutokana na ugomvi wa wazazi

Alibainisha kuwa kumekuwa na ongezeko la
wazazi wenzi kugombana majumbani na kufikia hatua ya kuwaonyesha watoto wao
tofauti zao kitu ambacho sio kizuri kwani unapo muonyesha mtoto tofauti zenu
wazazi ,mnawafanya waathirike na wakati mwingine badala ya kusoma wanawaza namna wazazi wanavyogombana .

“wazazi 
wengi sasa hivi wamekuwa wababe mnagombana kila mmoja anataka kuonyesha
ubabe wake mbele ya mtoto mkizani mnajenga lakini mnabomoa ,kwani kwanza
mnamuumiza mtoto kisaikolojia ,mnamuonyesha mtoto maadili mabaya ,na tabia
mbaya pia mnamfanya mtoto badala asome anaanza kuwawaza, nimeona hapa shuleni
kuna watoto wanamaliza leo darasa la saba lakini kutokana na tabia za wazazi wao
hawatamani hata kuondoka shule , wanafikia hatua yakusema mwalimu mimi bora
nibaki hapa hapa shule maana nyumba hapafai kitu ambacho sio kizuri na
kinawaumiza sana “alisema  Dinnah

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya
Arumeru Jerry Muro, Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe aliipongeza shule
hiyo kwa kuwalea watoto katika maadili mazuri na kuwapa elimu mbalimbali
ikiwemo ya kidini ,kimwili na kitaaluma ,ambapo pia alitumia muda huo
kuwasisitiza wazazi kuendelea kuwapa watoto hao waliohitimu  msingi mzuri wa kuendeleza vyema yale yote
waliofundishwa wakiwepo shuleni,.

Aliwasihi wazazi kutengeneza upendo wa kweli
na wanapokuwa na kasoro zao kutowashirikisha watoto kwani wanapowashirikisha  wanaweza kukabiliwa na matatizo mbalimbali ya
kisaikolojia ambayo huathiri uwezo wao wa kujifunza shuleni.

“wazazi mafanikio ya manafunzi ya kielimu na
kimaisha yamegawanyika kwa misingi mitatu ambayo msingi wa kwanza wa kumjenga
mwanafunzi ni  pale shuleni ambapo
anaposoma ambapo walimu wanamlea kwa asilimia 30,msingi wa pili ni mwanafunzi
mwenyewe ambaye yeye anachangia kwa asilimia 30, na asilimia 40 ambayo  imebaki ni ya mzazi sasa hapa mzazi usipo
fanya vyema kwa asilimia 100  inakuwa
umemuharibia mtoto maisha kiujumla hivyo ni jukumu la kila mzazi
kuhakikisha  anafanya vyema katika suala
la asilimia yake ili mtoto asifeli”alisema Mwaisumbe

Alimalizia kwa kuwataka wazazi kujenga tabia
ya kufuatilia watoto wao mashuleni  ili
kujua maendeleo yao shuleni na sio kuwaachia walimu tu kwani wanapowaachia
walimu wanawapa mzigo mkubwa .


Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shule ya  Trust St Patrick  schools Patrick  Thomas Khanya 
alisema kuwa jumla ya wanafunzi 76  wamehitimu darasa  la saba ,huku wanafunzi  41 wakihitimu kidato cha nne  tangu kuanzishwa kwa shule hiyo


Aliwataka wanafunzi hao  kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili waweze
kujitegemea wenyewe na sio kutegemea wazazi ,huku akiwataka wazazi kuwapa
watoto miongozo wa kimaisha  maana bado
ni wadogo na wanaitaji malezi yao mema ,Aidha aliwaonya wanafunzi  hao kutojiingiza katika masuala ya siasa
badala yake watilie mkazo katika elimu waliopewa na ambayo wataipata wakati
wakijiendeleza.