Uhakika wa maji unatokana na uhifadhi wa vyanzo vya maji bonde la wami/ruvu

Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo  ya Jamii na Mahusiano  wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  Horold Kayoza akizungumza na wanajumuiya
watumia maji wa Bonde la Wami/Ruvu pamoja na Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa
Mazingira (KIHUHWIZIGI) wakati wa ziara wa Jumuiya ya Bonde la Wami/Ruvu
kutembelea namna ya utunzji wa vyanzo vya maji katika msitu wa Amani wilayani
Muheza mkoani Tanga
Afisa Udhibiti  Ubora wa Huduma  na Mratibu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji
Safi na Mazingira jiji la Tanga (Tanga-Uwasa) Ramadhan Nyambuka akitoa maelezo
kuhusiana na namna walivyonufaika Mamlaka hiyo 
kutokana na jamiI kuwa na uthubutu wa kuhifadhi vyanzo vya maji.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima na
Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI , Twaha Mbaruku akizungumza kuhusiana na
umoja huo walivyopokea utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja kuinuka
kiuchumi wakati wa ziara ya Jumuiya ya Watumia maji wa Bonde la Wami/Ruvu.
Mwenyekiti wa Makinga Maji Mkazi
wa Kijiji cha Mbomole  Michael Simon
akieleza kwa waandishi wa  habari namna
ya makinga maji yanavyosaidia katika kuhifadhi vyanzo vya maji pasipo kuwepo
kwa udongo wa kutiririka ka vyanzo vya maji.
Maji yakitiririka msimu mzima wa
mwaka  katika Msitu wa Amani wilayani
Muheza.
Wanaumoja wa Wakulima na Uhifadhi
wa Mazingira KIHUHWIZIGI wakicheza ngoma za uhamasishaji wa Uhifadhi wa wa vyanzo
vya maji wakati wanajumuiya watumiaji maji wa bonde la Wami/Ruvu walipofanya
ziara katika  umoja huo namna
wanavyohifadhi vyanzo vya maji katika msitu wa Amani wilayani Muheza mkoani
Tanga
Mmoja wa wenye viti wa Watumia
Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Basley Matangaru akieleza namna walivyopata
elimu  ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo
vya maji  katika umoja wa Wakulima na
Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI.
Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa
Mazingira KIHUHWIZIGI wamejenga sehemu mahsusi kwa ajili ya kuonyeshea pikipiki
ili wasiweze kutiririsha uchafu katika vyanzo vya maji.
Mradi wa ufugaji samaki wa kikundi
cha hamasa ambacho kinasaidia kutojihusisha na shughuli za kilimo chenye
madhara katika vyanzo vya maji.
Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo  ya Jamii na Mahusiano  wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  Horold Kayoza akimkabidhi fedha taslimu
sh.100,000 kwa Katibu Msaidizi wa Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira
KIHUHWIZIGI Willium Masonda kwa ajili ya uhamasishaji wa uhifadhi wa vyanzo vya
maji kwa kikundi cha hamasa vhs umoja huo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii  Amani, Tanga
Katika kuendelea kuwepo kwa maji ya
uhakika na yenye usalama hakuna budi jamii kuhifadhi vyanzo vya maji
wanavyozunguka kwa kuendesha shughuli za kilimo zisizo na madhara katika vyanzo
hivyo.
Vyanzo ya maji vikihifadhiwa kwa
katika sekta ya kilimo kwa kupanda mazao ambayo hayana madhara katika
utiririshaji maji mamlaka husika kupunguza gharama za kutibu maji wakati wa
usambazaji wa maji hayo kwa wananchi.
Mkoa wa Tanga kwa wananchi
wanaozunguka vyanzo vya maji wameunda Umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira  Kihuhwizigi (Uwamasiki) ambao wamekuwa
wakihifadhi vyanzo vya maji na kufanya mamlaka 
ya Maji Safi na Mazingira jiji la Tanga Tanga Uwasa) kuunga mkono
jitithada za umoja huo.
Kutokana na Mamlaka ya Tanga kuwa
umoja wenye nguvu katika uhifadhi vyanzo vya maji Bonde la  Wami/Ruvu imepeleka jumuiya za Watumia Maji
katika vyanzo vya bonde hilo kujifanza katika umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa
Mazingira (Uwamasiki) ili kuleta chachu kuongeza mbinu katika uhifadhi wa
vyanzo vya maji.
Akizungumza wakati wa ziara ya
Jumuiya ya Watumia Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo  ya Jamii na Mahusiano  wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu  Horold Kayoza 
amesema kuwa wamepeleka jumuiya hizo kwenda Tanga kwenda kujifunza namna
Umoja wa Kilimo na Uhifadhi wa Mazingira (Kihuhwi) inavyolinda vyanzo vya maji
kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika vyanzo hivyo ikiwemo kilimo.
Kayoza amesema baada ya kutoka Tanga
nia ni kuona jumuiya ya watumia maji wanakwenda na kasi ya  kuweka mikakati ya kuhifadhi vyanzo vya maji
kwa kushirikisha wadau wote kwa kutumia elimu walioipata katika ziara ya Mkoa
wa Tanga.
Aidha amesema kuwa mazingira ya vynzo
vya maji katika mkoa wa Tanga havina tofauti na Mikoa ya Morogoro na  Pwani hivyo wanajumuiya ya watumiaji katika
Bonde la Wami/Ruvu watatumia mbinu mbalimbali walizozipata katika ziara ya
Tanga.
Nae Afisa Udhibiti  Ubora wa Huduma  na Mratibu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji
Safi na Mazingira jiji la Tanga (Tanga-Uwasa) Ramadhan Nyambuka amesema kuwa
kutokana na Umoja wa Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira (KIHUHWIZIGI) kuhifadhi
vyanzo vya maji kumeleta matokeo chanya kwa mamlaka kupunguza gharama za kutibu
maji.
Amesema kuwa wakati umoja huo ukiwa
haujaanzishwa walikuwa wanatumia gharama kubwa ya kutibu maji lakini kuanzishwa
kwa umoja huo Tanga-Uwasa limeendelea kupunguza gharama hizo ikiwa ni kuunga
mkono kwa ufadhili wa miradi kwenye umoja ili waendelee kutunza vyanzo vya
maji.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa
Wakulima na Uhifadhi wa Mazingira KIHUHWIZIGI , Twaha Mbaruku amesema kuwa
umoja umesimama vizuri kutokana na kila mmoja kujua umuhimu wa kuhifadhi vyanzo
vya maji.
Amesema wakati wanaanza umoja huo
kuna vyanzo vingine vilikuwa vimekufa lakini sasa vyanzo vyote vinatiririsha
maji wakati wote  huku shughuli za
kiuchumi zikiendelea bila kuathiri vyanzo hivyo.