Ujenzi wa mradi shirikishi wa miundombinu ya umwagiliaji waanza karagwe.

 

Mhandisi,
Meneja Umwagiliaji wa mradi shirikishi wa kilimo cha Umwagiliaji Mwisa
Wilayani Karagwe Bw. Adelialidy Mwesigwe akizungumza baada ya kupokea
baadhi ya vifaa vinavyotumika katika ukarabati kwenye skimu hiyo.

Picha Ikionesha sehemu ya Barabara katika Skimu hiyo kabla ya kuanza ukarabati.


Mwendesha
Mitambo Bw. Kuchada Faustine, akishindilia tuta kwa tumia mashine aina
ya (Hand Roller Compactor) wakati wa ukarabati katika skimu

 Kulia Meneja Mradi Shirikishi Mhandisi Adelialidy Mwesingwe akihakiki
baadhi ya vifaa vitakavyotumika katika ukarabati kwenye Skimu ya Mwisa
Wilayani Karagwe, kushoto ni Mpima Ardhi Bw.Ombeni Justo Ikola.

Na; MwandishiWetu, Karagwe–Kagera

Ukarabati
wa Miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji Wilayani Karagwe Mkoani Kagera
Umeanza Rasmi, kwa ujenzi wa Barabara katika skimu ya kilimo cha
umwagiliaji Mwisa pamoja na mifereji ya kupitisha maji kuelekea
mashambani.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa vya ujenzi
Mhandisi wa Umwagiliaji, ambaye pia ni Meneja Maradi huo shirikikishi
Bw.Adelialidy Mwesigwe, Amesema amepokea baadhi ya vifaa ambavyo
vitaweza kutumika katika ujenzi pamoja na kusakafia mfereji wenye urefu
wa mita mia saba hamsini (750).

Ambapo mpaka sasa mtaro wenye
urefu wa mita miatano na mbili (502) umeshachimbwa na barabara yenye
urefu wa mita mia saba na sitini (760) inayokwenda sambamba na mtaro huo
imekwishaandaliwa.

“Tutajenga vikinga maji tisa, (9)  kwenye
awamu hii kutokana na kwamba skimu hii inaukubwa wa eneo la Hekta
miatatu (300) ambalo linalimwa zao la mpunga na mazao mchanganyiko.”
Alisema Mwesigwa.

Aliendelea kusema kuwa eneo ambalo lipo nje
kidogo wakulima wanalima bustani za mboga mboga, na Skimu ina idadi ya
wakulima mia moja na sabini na tano (175).

Miradi hii
shirikishi ya maendeleo ya serikali ya awamu ya tano katika sekta ya
kilimo cha umwagiliaji inashirikisha wananchi wakazi waeneo husika
katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu hiyo.