Uulega watafiti toeni tafiti zenye majawabu ya changamoto za wafugaji ili kuleta tija yà uzalishaji wenye ubora

 Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi Abdallah ulega akifungua mkutano watafiti wa mifugo leo jijini Arusha.

 Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi katikati akiwa na Prof.Damian Kambarage na Prof. Hezron Nonga kwenye mkutano wa watafiti leo jijini Arusha

   Seh




 NaAhmed Mamoud,Arusha


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amewataka watafiti kufanya tafiti zitakazowasaidia wafugaji  na wavuvi nchini kujibu changamoto zinazowakabili na kuleta matokeo chanya

Aidha tatizo la minyoo bapa limeathiri mifugo kwa zaidi ya asilimia 60 kutokana na wafugaji wengi kutomudu gharama na uelewa mdogo wa kuwapeleka kwenye majosho

Ulega aliyasema hayo jana wakati akifungua kongamano la siku moja lililoshirikisha watafiti wa Chuo Kikuu cha Bristol(UK),Chuo Kikuu cha Liver pool na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA)

Alisema matokeo ya utafiti huo yameainisha athari na njia za kudhibiti magonjwa ya minyoo kwa mifugo na kuonyesha uwepo wa usugu wa vimelea vya magonjwa hayo kwa dawa zinazotumika kuua minyoo hiyo ambayo hushambulia kwenye ini la mnyama

Alisisitiza watafiti kutumia matokeo ya tafiti zao kwa ajili ya kutatua changamoto za wafugaji na mifugo badala ya kujinufaisha wenyewe huku wafugaji na wavuvi wakibaki bila kupata majibu

Naye Profesa Hezron Nonga Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, alisema magonjwa yatokanayo na minyoo yameonekana kupunguza uzalishaji hadi asilimia 10 kwa mifugo mfano ng’ombe mwenye minyoo anaweza kutoa maziwa kidogo

Alisema serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na magonjwa ya mifugo ikiwemo kugawa dawa za kuogeshea mifugo nchi nzima na kuzalisha chanjo za magonjwa ya msingi

Utafiti huo umeangazia kuwepo kwa usugu wa vimelea vya magonjwa ya minyoo kwa dawa zitakazotumika kutibu kwa sasa ambapo matokeo ya utafiti huo yaliwasilishwa kwa wakulima na wafugaji wa wilaya za Arumeru na Iringa na matokeo ya utafiti huo yamewasilishwa wizarani
Ili kuwezesha wataalamu na viongozi kuchukua hatua stahiki za kukomesha ugonjwa huo wa minyoo bapa