Umeme wawashwa mpimbwe

Meneja wa TANESCO mkoa wa katavi
Felix Olang’ akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Katavi; kulia ni Meneja
Mradi kutoka CRCEBG Arnold Nzali


Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homera akikata utepe kuashiria uzinduzi wa uwashaji umeme katika kata ya Maji Moto
…………………..
Na Mwandishi wetu,KATAVI
 
Zaidi ya wakazi 10,000 kati ya
wakazi 54,000 wa kata za Maji Moto na Mamba katika halmashauri ya
Mpimbwe mkoani Katavi wanatarajia kunufaika na huduma ya nishati ya
umeme baada ya kuwashwa kwa umeme katika kata hizo hii ikiwa ni mara ya
kwanza kuwashwa umeme katika maeneo hayo tangu kupatikana kwa uhuru
Wakizungumza na waandhishi wa
habari katika kampeni ya zima kibatari, zima jenereta, weka sola
pembeni, wananchi hao wameishukuru serikali kwa kuwapelekea huduma hiyo
Bwana Lameck Buzazi ni mmoja wa
wakazi wa kata ya Mamba amesema atatumia huduma hiyo katika mambo
mbalimbali ya kujiletea maendeleo
Baadhi ya vitu alivyotaja
anaweza kufanya kufuatia uwepo wa umeme ni pamoja na kufungua saluni ya
kiume, kununua jokofu kwa ajili ya biashara ya barafu kwa mkewe na
kuongeza kuwa kwa sasa hata uangaliaji wa runinga utakuwa wa uhakika na
hatasumbuka kufuata mpira katika runinga za maeneo ya baa
Mhandisi Felix Olang’ ni Meneja wa
TANESCO mkoa wa katavi, amesema wanaendelea kuwaunganisha wateja kwa
kushirikiana na mkandarasi wa kazi hiyo kutoka kampuni ya kichina ya
CRCEBG
 amesema katika tarafa ya maji moto wana transifoma 13 na mpaka sasa ni tatu ndio zimekwishaunganishwa na wateja.
 
kwa upande wake meneja wa
mradi kutoka kampuni ya kichina ya CRCEBG mhandisi Arnold Nzali amesema
ndani ya siku thelathini watakuwa wamekamilisha kuunga transifoma zote
13 mara baada ya kufanya zoezi la
uwashaji umeme katika baadhi ya makazi ya watu na kituo cha polisi maji
moto mkuu wa mkoa wa katavi bwana Juma Homera amezitaka taasisi za
serikali kuhakikisha zinajiunga na huduma hiyo.
Ametoa wito huo kufuatia kupokea
taarifa ya kusuasua kwa taasisi kujiunga na huduma ya nishati ya umeme
wa REA awamu ya tatu ambapo shule, zahanati, ofisi za serikali na
taasisi za dini kutochukua fomu za kuwekewa umeme

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *