Upelelezi kesi ya aliyemchoma moto mke wake wakamilika

Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili
Mfanyabiashara Khamisi Luwonga anaedaiwa kumuua Mkewe Naomi Marijani kwa
kumchoma kwa kutumia gunia mbili za mkaa umekamilika.


Wakili
wa Serikali Mwandamizi Simon Wankyo ameyasema hayo mbele ya Hakimu
Mkazi wa Mahakama hiyo Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipofikishwa
mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa, ambapo imepigwa kalenda hadi siku
ya Januari 7, 2020, itakapotajwa tena.


Mfanyabishara huyo, anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani
kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni, baada ya kumuua na kisha kumchoma
moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake na kisha kuyabeba mabaki ya
mwili huo na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.