Mamilioni
ya watu kaskazini mwa Uingereza wanakabiliana na sheria mpya ya
marufuku ya kutembeleana majumbani kufuatia ongezeko la maambukizi ya
virusi vya corona.
Sheria hiyo imeanza kutekelezwa mijini Manchester, mashariki ya Lancashire na sehemu ya magharibi mwa Yorkshire.
Katibu wa wizara ya afya ameiambia BBC kuhusu ongezeko la maambukizi kutokana na tabia ya watu kutembelea marafiki na ndugu.
Baadhi wamekosoa muda ambao tangazo hilo lilitangazwa kuwa majira ya jioni ya Alhamisi.
Katibu
wa wizara ya afya bwana Matt Hancock alisema taarifa hiyo ililenga watu
ambao walikuwa wamekutana na waliombukizwa kuacha kutembelea jamaa zao
ili kupunguza maambukizi.
Vivyo hivyo wamesitisha watu kujichanganya kwenye vilabu vya pombe, migahawa ingawa wataweza kutembelea maeneo ya hosptali.
Mabadiliko
hayo yamekuja wakati wa maandalizi ya sherehe za Eid na wiki chache tu
baada ya Uingereza kulegeza masharti yakei ya kuwaruhusu watu kukutana
nje tangu mwishoni mwa mwezi Machi.
Sheria hiyohiyo imewekwa Leicester, eneo ambalo kuna marufuku tangu mwezi uliopita.
Ingawa vilabu ,migahawa na maeneo mengine yanafunguliwa mjini kuanzia Jumatatu.#chanzo BBC