Waandishi
wa habari wanaoripotia redio Jamii (Mtwara), Ruangwa (Lindi), Pambazuko
(Ifakara), Chai (Rungwe), Ileje ( Songwe), na Kitulo (Makete-Njombe)
wakiwa kwenye kazi za makundi wakijadili namna ya kuandaa habari na
kuiwasilisha kwa kutumia miundo mbalimbali ya maudhui.

na watangazaji wa Redio za Kijamii nchini wameaswa kuzingatia
miiko,maadili na sheria zinazoongoza taaluma ya habari nchini ili
kulinda heshima ya taaluma yao.

Wito
huo umetolewa na mjini Morogoro na Mratibu wa mafunzo wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi Getrude John
wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya waandishi wa habari kutoka
redio za kijamii nchini.

Bi
Getrude alisema ni vyema waandishi na watangazaji wa redio za kijamii
wakatambua wajibu wao ndani ya jamii na hivyo kijibidiisha katika
kuielewa taaluma ya habari, misingi, weledi, sheria, mahitaji na matakwa
ya wasikilizaji wao pamoja na kuwajua wasikilizaji wao kiasili.

“Ukiwa
mwandishi wa habari za kijamii una wajibu mkubwa katika jamii yako na
hasa kuhakikisha unaijua jamii yako, hitaji lake pamoja na sheria na
maadili ya utangazaji na uandishi wa habari” alisisitiza Bi Getrude.

Alisisitiza
kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwa na changamoto nyingi za
kiweledi kwenye maudhui ya habari hususani redio za kijamii makosa
ambayo waandishi na watangazaji wa redio hizo wana nafasi kubwa ya
kuyarekebisha ili kuepuka makosa ya kisheria,kimaadili na kushindwa
kutengeneza maudhui yanayotengeneza jamiiyenye mtazamo chanya,yenye
ubunifu na inayozingatia maadili ya jamii husika.

“Kazi
ya uandishi wa habari ina maadili na sheria zake, ina miiko
inayoiongoza,bila kuijua unaweza kujikuta unaingia kwenye mgogoro na
jamii unayoihudumia”

Kwa
upande wao washiriki wa mafunzo hayo wameomba UNESCO kuyaendeleza
mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo kutokana na walio wengi kukosa nafasi
ya kupata mafunzo ya uandishi wa habari kabla ya kuanza kufanya kazi na
redio za kijamii.

“Sisi
wengi tunaofanya kazi na Redio za kijamii,hatukubahatika kupitia katika
mfumo rasmi wa elimu ya habari, tunaomba tupatiwe mafunzo zaidi ya haya
ili tuwe na utaalamu na maarifa yatakayotufanya tuandae maudhui
yanayojibu changamoto ya jamii tunazozihudumia huku tukizingatia maadili
na sheria” alisema Tumain Obel kutoka Redio Chai FM.

Jumla
ya waandishi 24 kutoka redio 6 za kijamii kutoka Tanzania Bara
wanahudhuria mafunzo ya siku tano yanayoratibiwa na kuendeshwa na UNESCO
chini ya mradi wa SDC yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi na
watangazaji wa redio za kijamii kwenye eneo la maadili, sheria, ujuzi na
weledi katika taaluma ya habari.

Mafunzo
kama haya yalifanyika wiki iliyopita visiwani Zanziar kwa kuhusisha
waandishi na watangazaji wa redio za kijamii 16 kutoka vituo 4 vya redio
za kijamii kutoka Unguja na Pemba.