Wabunge wanne wa chadema wafukuzwa uanachama

“Kamati Kuu CHADEMA imeazimia Wabunge Anthony Komu na Joseph Selasini pamoja na kuwa wamejipotezea sifa ya uanachama wa CHADEMA, wameendelea kutoka kauli za kejeli, kashfa na kukiuka maagizo ya Chama, hivyo Chama kimeazimia kuwafukuza uanachama” -John Mnyika, Katibu Mkuu CHADEMA

“Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare sio tu wamekiuka agizo la Chama bali wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama, Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama”- MNYIKA

“Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA,  Mariamu Msabaha, ameshiriki kukiuka maagizo ya Chama, ilitakiwa awe mfano na kwakuwa amekwenda kinyume, amevuliwa nafasi zake zote ndani ya Chama na kubaki na Ubunge na atatakiwa ajieleze kwanini asichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo”-MNYIKA

“Kuhusu Wabunge wengine ambao wamekwena kinyume na maagizo ya Chama lakini hawajaonesha utovu wa nidhamu kwa kutoa kashfa kwa Chama, watatakiwa wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo” -MNYIKA
John Mnyika apewa ziara na Wizara | East Africa Television