Wagombea 1,851 wa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa mkoani rukwa

Wagombea
wa vyama vya upinzani wapatao 1,851 kushiriki katika nafasi mbalimbali
za uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nchini tarehe 24.11.2019
ili kuwapata wawakilishi katika ngazi ya kijiji, mtaa, kitongoji pamoja
na wajumbe mchanganyiko na wajumbe wa viti maalum katika ngazi hizo.


Taarifa
kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa inasema kuwa wagombea hao
hawatakuwa na uwezo wa kuweka mawakala kisheria kwasababu mawakala hao
wanatakiwa kuwa na kiapo cha kisheria pamoja na utambulisho kutoka kwa
wasimamizi wa uchaguzi na kuongeza kuwa ni isipokuwa mgombea mwenyewe
ndiye anaweza kuwa wakala.

Aidha,
ametahadharisha kuwa endao kutatokea vurugu katika maeneo ambayo
kwasababu nembo ya chama cha upinzani imetumika wakati mgombea amejitoa
ambapo yawezekana alijitoa kwa kuchelewa au aliamua kutosumbuka
kujitoa,Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zitaimarisha ulinzi katika
maeneo ya kupiga kura.

Idadi
ya wagombea wa vyama vya upinzani waliobakia Mkoani Rukwa baada ya
mwisho wa tarehe ya kujitoa 16.11.2019 saa 10 jioni ni katika vijiji 67
(19.7%), Vitongoji 348 (19.1)%, mitaa 9 (5.4%), wajumbe mchanganyiko 876
(11.8%) na wajumbe wa viti maalumu 551 (19.1%). Mkoa una jumla ya
vijiji 339, vitongoji 1,817, mitaa165. Wajumbe mchanganyiko 7,420 na
wajumbe wa viti maalum 2,875.