Wanafunzi wajeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani

Wanafunzi 39 wa darasa la nne shule ya Msingi Ihumilo wilayani Geita wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani.
 Radi

Mganga
mfawidhi wa hospitali ya wilaya Kaitila Murusuri ,amesema walipowakea
wanafunzi 24 saa mbili asubuhi na kuwapatia huduma ya kwanza. 
”Tumepokea
gari ya dharura kutoka zahanati ya karibu ya mkoma ikiwa imebeba
wanafunzi wa shule ya msingi wapatao 24 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na
ajali ya kupigwa na radi , tulipowafanyia uchunguzi wengi wao walikuwa
katika hali ya kawaida, tuliporidhika tuliwaruhusu lakini tulibaki na
wengine watano, kikubwa ni kwamba walipata mshtuko”. Alieleza daktari
Murusuri.
Taarifa
zimesema radi hiyo imesababisha watoto kupata mshtuko na kuzimia lakini
baada ya kupatiwa huduma ya kwanza kwa sasa wanaendelea vizuri na
tayari wengi wao wameruhusiwa kutoka hospitali.
Taarifa zinasema
kuwa majira ya saa moja asubuhi ilipiga radi kali katika shule iliyopo
maeneo ya Nzera katika halmashauri ya wilaya ya Geita. Watumishi wa afya waliwahi kuwasaidia kupata huduma ya kwanza.
 Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel

Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel amesema amezungumza na watoto hao wa darasa la nne.

”Ni
majira ya mvua kipindi hiki radi hupiga wakati wote ukiwa barabarani
radi inakufuata, ukiwa kwenye jengo lenye umeme radi inapiga, ukiwa
kwenye jengo la umeme, kukiwa hakuna umeme radi inapiga kuna teknolojia
inapaswa kutazamwa kuona ni namna gani tunaweza kujikinga na radi katika
majengo yetu”. Amesema mkuu huyo wa mkoa.

 BBC