Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema
mabweni mawili ya wanafunzi maarufu kama “hall 5 na hall 2 “katika Chuo kikuu
cha Dar es Salaam yaliyokarabatiwa yatachukua wanafunzi 788 .

Ndalichako amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi
ya ukarabati wa Mabweni, Vyumba vya mihadhara na Ofisi katika Ndaki ya
Uhandisi Katika Chuo hicho.
Mabweni
hayo, yanakarabatiwa na Serikali kwa Shilingi za Tanzania zaidi ya
Bilioni 4.5, ukarabati ukihusisha kuweka upya mifumo ya maji safi na
taka, mifumo ya umeme, kuwekwa upya makabati na milango mipya,
madirisha uwekaji vigae vipya vya ukutani na uwekaji “lift” mpya.
Ukarabati
huu unatarajiwa kukamilika, ifikapo mwezi Oktoba, 2019. unatekelezwa
na Mkandarasi SUMA JKT- na kusimamiwa na kurugenzi ya milki ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na ulianza 2018. Mabweni haya yalijengwa mwaka
1965 na kwa mara ya kwanza yanafanyiwa ukarabati mkubwa baada ya
kusitisha utumiaji kutokana na uchakavu.
Waziri
Ndalichako amepongeza kasi na ubora wa kazi ya ukarabati huo, huku
akipongeza hatua ya chuo Kikuu kutumia wataalamu wake wa ndani kusimamia
kazi za ukarabati katika chuo hicho.
“Nimefurahishwa
na kazi hii ni bora na kasi ya kazi ya ukarabatiwa mabweni haya kwani
yataongeza uwezo wa chuo kutoa huduma ya Malazi kwa wanachuo zaidi ya
11,100. Naagiza uongozi mko hapa maagizo kwa hakikisheni ukarabati wa
mabweni haya na majengo katika Ndaki ya Uhandisi unakamilika kabla ya
kufunguliwa Chuo Novemba ili isiwe bugudha kwa wanafunzi, Mwaka huu ”
Akimkaribisha
Waziri wa Elimu, Makamu Mkuu wa Chuo Cha Dar es salaam Profesa Wiliam
Anangisye ameishukuru Serikali ya awamu ya tano na Waziri wa Elimu kwa
kutekeleza kwa vitendo azma ya kuboresha ili ili kuhahakikisha vijana
wanapata elimu katika mazingira bora. Amemuhakikishia Waziri Ndalichako
kuwa Chuo kitasimamia na kuhakikisha kazi zinazoendelea zinakamilika
kwa wakati .
“
tunaishuruku serikali ya Awamu ya Tano na wewe Mheshimiwa kwani
maendeleo haya ni maono ya Serikali na yanatekelezwa na serikali , nasi
tunakuhakikishia pia kuendelea kutunza miundo mbinu hii na kutumia
mapato ya ndani kuyaendeleza”
Nae
Dkt. Liberato Haule Mkurugenzi wa Mipango Uwekezaji na Maendeleo
akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi amezungumzia ukarabati wa majengo
ya Ndaki ya Uhandisi kuwa umefikia asilimia 45 na kuwa utagharimu
shilingi bilioni 1.5 .
“
napenda kutoa taarifa kuwa mradi wa ukarabati wa majengo ya Ndaki ya
Uhandisi unahusisha majengo ya ofisi na madarasa, nyumba za wafanyakazi
na bweni moja lililopo kitalu G. nikuhahakikishie Mh Waziri kuwa
mataraji yetu ni kuwa kazi itakamilika kwa wakati uliopangwa Novemba
mwaka huu“
Nae
Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) Bi. Jackline Ndombele,
ameishukuru serikali kwa ukarabati mkubwa unaoendelea hall 5 na hall 2
na kwamba utasaidia sana kuongeza idadi ya wanafunzi wanaokaa chuo,
kwani kwa sasa wengi wanakaa nje ya Chuo.

wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (wa pili
kulia), akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ukarabati wa majengo ya
Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET), Prof. Aloyce Mayo, wakati wa
ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya ukarabati wa mabweni mawili ya
wanafunzi pamoja na mfumo wa kusambaza majisafi katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam
Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikagua
mabweni yanayokarabatiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako katika ukaguzi wa mabweni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Picha mbalimbali za ukaguzi wa majengo yanayokarabatiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.