Wanawake wawili kenya wabadilishana waume zao

 Na Mwandishi Wetu, Kenya

Wanawake wawili kutoka kaunti ya
Busia, magharibi mwa Kenya wamewaacha watu na bumbuwazi mara baada ya
kubadilishana waume zao kwa lengo la kutafuta furaha.
Lilian Weta
mwenye umri wa 28, mama wa watoto watatu na Millicent Auma mwenye umri
wa miaka 29, mwenye watoto wawili wamezua gumzo katika mtandao nchini
Kenya kwa kuonekana kuwa wamefanya jambo la ajabu sana kwa wanandoa hao
kuamua kubadilishana wenza.
Wiki moja iliyopita wapenzi hao
waliandikishiana serikalini namna watoto watalindwa baada ya wanawake
hao kubadilishana waume zao pamoja na watoto.
Wanawake hao wanadai walifikia maamuzi hayo baada ya kusukumwa na ugomvi usioisha katika familia zao.
Vyombo
vya habari vya Kenya vimemripoti Lilian akisema alifikia uamuzi huo
mara baada ya mume wake kumleta mwanamke mwingine katika nyumba yao
,mwezi mmoja uliopita.
“Mume wangu alinidanganya kuwa binamu yake
kutoka Bungoma anakuja kututembelea hivyo niandae chakula, na sehemu ya
kulala mgeni. 
Muda mfupi tu ulipita kuna mwanamke aliingia na kuniambia
nimuachie nafasi kwa sababu hiyo ni nyumba yake sasa au anidunge kisu,”
Lilian alisema.
Lilian aliendelea kusimulia kuwa Auma alimwambia
akamtafute mume wake na akimpata aoleke huko na kweli alimtafuta mume wa
Millecent na kwenda kufunga ndoa halali wiki tatu zilizopita.
“Mwanamke huyu alikuja akilia na kulalamika kuwa mke wangu amemchukua mume wake na nyumba yake,”
“Nilimwambia kwamba kama mke wangu ndio amekufukuza kwako basi
nenda ukachukue mizigo yako na watoto na uje ukae na mimi hapa,”
alisema Bwire ambaye alikuwa mume wa Millecent.
Ni wiki mbili sasa
Lilian Weta alipoolewa na Christopher Bwire baada ya wapenzi wao
kuwasaliti na wanadai kuwa hawajutii kitendo walichokifanya.
Bwire ameviambia vyombo vya habari nchini humo jinsi maisha yake yalivyobadilika na kuwa ya furaha.
“Wabaya wawili wapatane na wawili wazuri wapatane, sina msongo wa mawazo. Siku hizi ninaamka muda ninaotaka na kulala muda ninaoaka ninakula vizuri, nina furaha sana kuwa na Lilian,” alisema Bwire. 
Na upande wake Lilian pia anadai kuwa ana furaha sana kukaa na Bwire.
Barasa
ambaye ni mume wake Lilian zamani anasema kuwa hana haja ya kumfuata
mke wake na hataki kujua chochote kumuhusu kwa sababu yeye na Auma wana
furaha sana.