Naibu waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua Mkutano wa mwaka na kongamano la Kisayansi la chama chaMadaktari wa mifugo Tanzania (TVA).
Zingine zote ni picha za washiriki wa mkutano wakifuatilia mada na hotuba za ufunguzi wa mkutano huo mapema leo.
Prof. Robinson Mdegela ambaye ni mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA akiwasilisha mada juu ya dhana ya afya moja kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda na Mweyekiti wa Kikao hicho akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo kwenye ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Matamwe Said akitoa neno kabla ya Kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kufungua mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania (TVA) Prof. Dominic Kambarage akieleza malengo ya Mkutano huo wa Kisayansi mbele ya Mgeni Rasmi.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Watafiti nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa tafiti wanazofanya zinasaidia katika kutengeneza sera au kuziboresha ili kutoa mchango wa moja kwa moja kwa jamii na taifa badala ya kuishia kwenye makabati na machapisho ya kimataifa.
Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua Mkutano wa mwaka na kongamano la Kisayansi la chama chaMadaktari wa mifugo Tanzania (TVA) uliokutanisha wadau wote wa Afya moja kutoka wizara,Taasisi za elimu ya juu,Taasisi za utafiti,Mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali kutoka Tanzania na nje ya Tanzania uliofanyika kwene ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Dkt.Ndugulile amesema Kuna tafiti nyini zinafanywa nchini lakini zinaishia kwenye machapisho ya kimataifa lakini ifike wakati matokeo mazuri ya kazi nzuri za utafiti zinazofanywa wa watafiti nchini ziweze kuisaidia serikali kutunga sera nzuri ambazo zitatengeneza miongozo mizuri ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.
”Niwapongeze sana TVA kwa kufanya mkutano huu mkubwa wa kwanza nchini unaowakutanisha wadau wengi wa dhana ya afya moja kutoka sekta mbalimbali na ni matumaini yangu na ya serikali kuwa kwa mjumuiko huu mkubwa wa watafiti mtakuja na mapendekezo mazuri ambayo yataisaidia serikali kufanya maamuzi sahihi kwenye kutelekeza dhana hii ya afya moja” Aliema Dkt.Ngugulile.
Naibu huyo wa Wizara ya afya amesema ulinzi wa afya ya Binadamu,mimea na wanyama unahitaji ushirikiano wa wadau wote na kwamba Serikali tayari ilishaanza kutekeleza mpango huu kwa kuanzisha dawati la afya moja kwenye ofisi ya waziri mkuu ambalo linasaidia kuratibu utekelezaji wa dhana hii ambayo sasa ndio ajenda ya dunia kwa umuhimu wake.
”Niwaombe elimu hii ambayo mnaitoa katika ngazi ya kitaifa ifike hadi kwenye ngazi za serikali za mitaa kwa kuwashirikisha wadau wengi zaidi katika ngazi hiyo kwenye sekata mbalimbali ili nao wapate uelewa ili iwe rahisi kwenye utekelezaji wa mpango mkakati huu wa kidunia ambao kitaifa uliziduliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mwaka 2015” Alisisitiza Naibu waziri wa Afya Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile.
Mhe. Ndugulile ametaka kuwepo kwa takwimu za kina kuhusu masuala ya Afya moja hapa nchini kutokana na kuwepo kwa wadau mbalimbali wanaofanya kazi hiyo ili takwimu hizo zisaidie serikali kwenye kufanya maamuzi ya vipaumbele katika kuwekeza fedha zake maana bila hivyo ni ngumu kuishawishi serikali
kufanya maamuzi.
kufanya maamuzi.
Akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua Mkutano huo
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Matamwe Said amesema umuhimu wa Dhana ya afya moja kwa taifa ndiyo imeifanya serikali kuona umuhimu wa kuanzisha dawati kwenye ofisi ya waziri mkuu ambalo limeleta mafanikio makubwa katika mkakati huu ambao ndio ajenda ya dunia kwa sasa.
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Matamwe Said amesema umuhimu wa Dhana ya afya moja kwa taifa ndiyo imeifanya serikali kuona umuhimu wa kuanzisha dawati kwenye ofisi ya waziri mkuu ambalo limeleta mafanikio makubwa katika mkakati huu ambao ndio ajenda ya dunia kwa sasa.
Amesema kuwa Mabadilio ya tabia nchi yanapelekea kuwepo kwa magonjwa kwa mimea,Wanyama na Binadamu ambayo sasa yanahatarisha afya hivyo ni muhimu wadau wote kwa pamoja wakaweka mikakati ya pamoja kwa kushirikiana na dawati ili kuboresha afya za binadamu.
Kanali Said amesema Mkutano huu ulioandaliwa na TVA na kuratibwa na ofisi ya Waziri Mkuu ni mwanzo wa mikutano mingi ambayo itafuata ya kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja kwa sekta zote ili kutimiza mpango wa dhana ya Afya moja nchini.
Nae kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania (TVA) Prof. Dominic Kambarage amesema kwa mara ya kwanza TVA imefanya kongamano la aina hiyo la kisayansi ambalo limelenga kwenye mada moja ya dhana ya afya moja na kuwakutanisha wadau wote katika ngazi zote.
Amesema linapotokea tatizo la ugonjwa wa mifugo wanaofanya kazi hiyo ni madaktari wa mifugo lakini kwa kuwepo kwa magonjwa sita makubwa yanayoambukizwa kati ya binadamu na wanyama kuna kila sababu ya kuwepo kwa ushrikino wa pamoja maana matatizo hayo yanagusa wataalamu wa aina tofauti tofauti katika kuyatatua.
” Zaidi ya asilimia 70 ya magonjwa ya Binadamu vyanzo vyake ni kutoka kwa Wanyama na wanyama na serikali inatumia fedha nyingi kwenye kutibu ugonjwa unapotokea hivyo ni wakati sasa umefika wataalamu wakaanza kushirikiana ili kukinga wanyama na adhari zinazoweza kutokea kwa bidamu kama ilivyo kwa magonjwa kichaa cha mbwa” Alisema Prof. Kambarage.
Prof. Kambarage ametoa wito kwa jamii kuacha kulala ndani na mifugo yao ili kuepuka kupata maambukizi ya magonjwa hayo yasiyo na lazima lakini pia kuipatia kinga mifugo yao pale inapotakiwa kwa wakati.