Watanzania tumuunge mkono rais wetu mhe.samia suluhu-bw.festo

 

 Kijana
Mzalendo Bw.Frank Festo (Kulia)akiwa pamoja na rais wa Chuo cha Bahari
(DMI) Bw.Salim Awali wakionesha stika yenye ujumbe “MIMI NASIMAMA NA
MAMA SAMIA,WEWE JE”.


Kijana
Mzalendo Bw.Frank Festo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
leo Jijini Dar es Salaam baada ya kukutana kwaajili ya uzinduzi wa stika
yenye ujumbe “MIMI NASIMAMA NA MAMA SAMIA,WEWE JE”.


(Picha na Emmanuel Mbatilo)




NA EMMANUEL MBATILO


Ili
kuweza kuunga mkono Juhudi za Rais Mhe.Samia Suluhu Hassani, Kijana
Mzalendo Bw.Frank Festo amezindua stika yenye ujumbe “MIMI NASIMAMA NA
MAMA SAMIA,WEWE JE”. Lengo kuhamasisha mshikamano, umoja, upendo, amani
na furaha kama kipaumbele cha Rais Mhe.Samia Suluhu.


Akizungumza
na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Bw.Festo amesema sote kwa
pamoja tunapaswa kumuunga mkono ili kuweza kufanikisha kuiongoza
Tanzania katika amani na upendo tulionayo toka zamani.


“Tusikae
pembeni kwa kuchungulia na kumsikiliza eti huyu mama ataweza?.Kila
mmoja awajibike kwa nafasi yake ipasavyo ndiyo njia pekee ya kumuunga
mkono Mama yetu mpendwa”. Amesema Bw.Festo.


Aidha
Bw.Festo amesema stika hiyo itasambazwa nchi nzima kupitia vyombo vya
habari, mitandao ya kijamii, vyombo vya usafiri, kutembelea ofisi za
Umma na Binafsi,Bunge, Shule,Vyuo na nyumba za ibada ikiwa lengo ni
kuhakikisha ujumbe huo unamfikia kila mtanzania mahali popote alipo.


Pamoja
na hayo Bw.Festo amesema kuwa pamoja na taifa letu kujaliwa rasilimali
nyingi, rasilimali kubwa tuliokuwa nayo ni amani na hatuna mbadala wa
amani.


Kwa
upande wake rais wa Chuo cha Bahari (DMI) Bw.Salim Awali amewasihi
viongozi ambao wamepewa dhamana serikalini kufanya kazi kwa bidii bila
kumkatisha tamaa Rais kwa masirahi ya nchi yetu.


“Sisi
kama vijana tunamuahidi Rais wetu tutaliendeleza taifa hili kwa umoja
na kumshauri ni nini kifanyike ili tuweze kufika sehemu ambayo tunaitaka
kwasababu kiongozi wetu Rais Mhe.Samia ni mtu ambaye anapokea ushauri
na ni mtu ambaye msikivu”. Amesema Bw.Awali.