Watu 6 wafikishwa mahakamani na takukuru kwa uhujumu uchumi

Taasisi
ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Jeshi
la Polisi, Jumatano Novemba 20, imewakamata na kuwafikisha mahakamani
wafanyabiashara sita wakiwamo raia wa kigeni kutoka nchini China kujibu
mashtaka ya Rushwa na uhujumu uchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi), Wli Mfuru amewataja watuhumiwa hao
waliofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha mkoani Pwani kuwa
ni You Hattao, Zhang Zhi Xin wote raia wa China, wengine ni John Mnyele,
Loncolin Ilungu, Andrew Kowelo na Emmanuel Maro, ambao wote ni
watanzania.
 

Amesema
watuhumiwa hao wamekuwa wakimiliki kampuni maeneo ya Kibaha
inayotengeneza na kuuza mafuta aina ya Dizeli yaliyo chini ya kiwango na
kuyauzia baadhi ya kampuni zinazofanya biashara hiyo bila kufuata
taratibu za ufanyaji biashara.


“Uchunguzi uliofanywa na Takukuru kwa kushirikiana na jeshi la polisi
limebaini kampuni ya SHIN UP iliyopo Visiga imejihusisha na vitendo vya
rushwa pamoja  na uhujumu uchumi na kusababisha serikali hasara ya zaidi
ya 1.2 bilioni,” amesema Mfuru
“Pamoja na mambo mengine, kampuni hii imeghushi vyeti vya kuwawezesha
kufanya biashara nchini, inakwepa kodi pamoja na watuhumiwa kujihusisha
na mtandao wa uhalifu,” alisema
Amewataja watuhumiwa hao ni Yu Hattao na Zhang Zhi ambao wote ni raia wa
China, John Mnyele, Lincolin Ilungu, Andrew Kowelo na Emmanuel Maro
ambao ni Watanzania.
Mfuru amesema Oktoba 3O, 2019 Takukuru iliwafikisha mahakamani
watuhumiwa watatu kati ya hao ambapo washtakiwa wengine wameeunganishwa
nakuongezewa mashtaka yakiwemo utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.